#Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasiasa wa kwanza kutoka nchini - TopicsExpress



          

#Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasiasa wa kwanza kutoka nchini Tanzania kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Asha-Rose Mtengeti Migiro ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Amepewa cheo hiki na Katibu Mkuu Ban Ki-moon tar. 5 Januari 2007. Hadi kuteuliwa kwa cheo cha UM alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania tangu Januari 2006. Wajibu huo alipewa na rais Jakaya Kikwete aliyemteua kumfuata katika wizara ya mambo ya nje iliyoshikwa awali na Kikwete mwenyewe. Chini ya raisi Benjamin Mkapa Migiro alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Alikuwa mbunge kwa njia ya kiti maalumu cha wanawake. Kabla ya kujiunga na siasa alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alisoma digrii za bachelor na master Dar es Salaam. Mwaka 1992 akaongeza cheti cha udaktari wa sharia kwenye Chuo kikuu cha Konstanz (Ujerumani). Akarudi Tanzania alipoanza kufundisha. Akawa mwanachama wa CCM Akiwa Mwislamu ameolewa na Cleophas Migiro wana watoto wawili wa kike.
Posted on: Tue, 19 Nov 2013 13:41:43 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015