﹑﹑ ENDELEA KUISOMA HII STORY YA KWELI LEO NIMEAMBATANISHA - TopicsExpress



          

﹑﹑ ENDELEA KUISOMA HII STORY YA KWELI LEO NIMEAMBATANISHA ANZA YA NYUMA ﹑﹑ Ilipoishia Johnson aliwahi asubuhi kama kawaida yake akaanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda gengeni kwake akamwambia Maria awahi kwenda kwao kabla wazazi wake hawajarudi Endelea Johnson aliondoka huku anamsisitizia sana Maria asibaki pale nyumbani kwake asubuhi ile ile ajiandae arudi nyumbani kwao akaondoka akamuacha Maria bado kalala Alifika gengeni kwake akafungua akaanza kupanga panga bidhaa zake alivyomaliza akachukua simu yake akampigia Maria akamuuliza vipi mpenzi wangu umeshaondoka?? Maria akamjibu bado nipo kwako mpenzi ila nimempigia housegirl simu kaniambia nyumbani kupo shwari wala hamna tatizo Johnson alikasirika sana kusikia vile akamwambia Maria hata kama umempigia mfanyakazi wenu simu we jiandae uondoke hapo usije ukaniletea matatizo mimi wazazi wako wanaweza kurudi mda wowote plz nenda kwenu uje siku nyingine Maria alivyoona Johnson kabadilika akamwambia sawa mpenzi nimekubali naenda nyumbani ila nikiona hadi jioni wazazi wangu hawajarudi nitakuja tena kulala na wewe huku kwako Johnson akamwambia we katulie kwanza mimi najua hapo wazazi wako wamekutega tu hawawezi kukuambia watarudi lini wala saa ngapi wanataka wakustukize sasa ukija kulala huku wakirudi ghafla wakute hujalala kwenu itakuwa balaa Johnson alimuelewesha Maria hadi akamuelewa yeye akaendelea na shughuli zake huku akiwa na amani sababu Maria alimsikiliza alivyomwambia arudi nyumbani kwao Mzee Joseph alienda kukaa na Johson pale gengeni kwake wakawa wanapiga stori akamuuliza Johnson vipi yule mpenzi wako sasa hivi mnaenda sawa?? Johnson akaguna akamjibu Yani mzee nakushukuru sana kwa yale maneno uliyompa siku ile hapa gengeni sasa hivi kidogo kajirekebisha hanifwati tena hapa gengeni kwangu hata nyumbani kwangu haji ovyo ile jana ndo ilikuwa majanga Mzee Joseph akamuuliza Johnson Majanga gani tena kijana wangu?? Johnson akamwambia jana mda ule natoka huku gengeni usiku ule nilimkuta nyumbani kwangu kalala nilichanganyikiwa nilivyomuuliza kwanini yupo pale usiku wote ule akanijibu wazazi wake hawapo wamesafiri wameenda msibani nikalala naye ila nimemwambia arudi kwao mapema kabla wazazi wake hawajarudi Mzee Joseph akacheka sana akamwambia Johnson we kijana sijui umempa nini yule binti yani na uzuri wake wote ule na elimu yake na utajiri wa kwao lakini kafa kaoza kwako wewe muuza genge una bahati sana kijana wenzako hizo bahati wanazitafuta kila kukicha hawazipati sasa inabidi umtumie vizuri yule binti atakutoa kimaisha Johnson alistuka kidogo akamuuliza mzee mbona sijakuelewa mzee atanitoa kimaisha kivipi?? Mzee akacheka akamwambia hapa mjini kijana wangu watoto wa kishua kama wale wanaweza wakakufanya uache kuuza genge hapa ufanye biashara kubwa wanaweza wakakufanya uwe na pesa kupitia zile zile pesa za nyumbani kwao Johnson akabaki anashangaa tu Inaendelea GONGA LIKE KAMA UMEIPENDA HII STORY
Posted on: Sun, 20 Oct 2013 08:54:23 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015