::: HABARI 10 ZA USAJILI ZILIZOBAMBA KATIKA MAGAZETI YA ULAYA JANA - TopicsExpress



          

::: HABARI 10 ZA USAJILI ZILIZOBAMBA KATIKA MAGAZETI YA ULAYA JANA - ALHAMISI::: 1) Meneja wa zamani wa Chelsea, Milan na PSG Carlo Ancelotti amechukua rasmi mikoba ya kuikochi Real Madrid na ana shauku la kufanya chochote awezacho kuzuia staa Ronaldo asiondoke klabuni hapo. Kuna tetesi nzito zinazomuhusisha Ronaldo kuihama klabu hiyo tokea mwanzo wa mwezi Desemba mwaka jana na kurudi klabu Old Trafford. Licha ya rais wa Real Florentino Perez kusisitiza Ronaldo atasaini mkataba mpya kurefusha alionao sasa, ripoti kwenye vyombo vya habari vinadai kwamba staa huyo wa ki-Portugal atakutana na wakurugenzi wa United wiki hii kuongelea uwezekano wa kuhamia klabu hiyo. Lakini akiongea siku aliyotambulishwa rasmi Bernabeu, meneja Ancelotti alikua akisisitiza kwamba Ronaldo ndiye tegemeo la mipango yake yote kuipatia Madrid kombe la 10 la Champions League..(The Sun) 2 ) Mchezaji bora wa msimu uliopita Chelsea Juan Mata ametupilia mbali uvumi kua anataka kurudi kuchezea timu za nyumbani kwake - Spain kwa dau linalofikia £35milioni. Real Madrid na Barcelona zikihusishwa na mpango mzima.(Dail Mirror) 3 ) Kutua kwa meneja mpya klabuni Ral Madrid na Juve kumsajili Tevez kwa £10million kunamsukuma zaidi Gonzalo Higuain kujiunga na Arsenal. Straika huyo wa Madrid amekubaliana na mshahara wa £125,000 kwa wiki na the Gunners, ukimfanya kua juu ya wanaolipwa zaidi sasa klabuni hapo Jack Wilshere, Theo Walcott na Lukas Podolski. Kwa sasa inasubiriwa dili la £22m kuidhinishwa na bosi mpya wa Real Carlo Ancelotti. Higuain, 25, amekua windo la muda mrefu la Juventus. Lakini kaka wa Higuain ambaye pia ndiye wakala wake aitwaye Nicolas amethibitisha kwamba baada ya Tevez kusajiliwa na Juve kwa kua hawakua na pesa za kutosha kumnunua Gonzalo, staa huyo wa Argentina njia ipo wazi kujiunga na Emirates muda si mrefu. (The sun) 4 ) Liverpool wameambiwa kama wanataka lazima watoe £25m ndani ya siku 10 iili kumsajili kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 24 Henrikh Mkhitaryan kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk.(the Sun) 5 ) Liverpool wanataka kufanya maongezi ya dharura na straika wao anayelekea kuwaponyoka Luis Suarez, 26, kupima kama kwa namna yoyote amevunja makubaliano yaliyomo ndani ya mkataba wake na klabu hiyo ya kutokufanya mazungumzo na klabu yoyote mpaka timu hiyo itoe idhini kufuatia tetesi kutoka Spain kwamba amefikia makubaliano binafsi na Real Madrid.(Daily Telegraph) 6 ) Ingawa kuna kila dalili kuonesha kwamba Arsenal wamekamilisha taratibu za kumnasa straika Higuain, hawajaishia hapo kwani wametenga au nono kumshawishi straika wa Manchester United Wayne Rooney, 27, kujiunga Emirates. Viongozi wa juu wa klabu hiyo wanaamini usajili wa mchezaji kama Rooney kutamshawishi meneja wao wa sasa Arsene Wenger ambaye anawindwa bado na PSG kusaini mkataba wa kuongeza muda na the Gunners. (Daily Star) 7 ) Swansea wanataka kumsajili kiungo wa Liverpool mwenye miaka 21 Jonjo Shelvey lakini watatakiwa walipe angalau £5m kukamilisha dilil. (Daily Mirror) 8 ) Manchester City wanataka kumtoa straika wao mwenye miaka 27- Edin Dzeko na pesa kwa Borussia Dortmund kama sehemu ya dili la kumleta mshambulizi Robert Lewandowski, 24, klabuni Etihad.( Daily Express ) 9 ) Real Madrid wameofa fedha na mchezaji - dili likimjumuisha winga mu-Argentina mwenye miaka 25 Angel di Maria - kwa Tottenham katika jaribio la kumsajili Gareth Bale kwa ajili ya bosi mpya wa klabu hiyo Carlo Ancelotti.. (Daily Star) 10 )Real Madrid wamethibitisha usajili wa windo la muda mrefu la Manchester City Isco kutoka klabu ya Malaga. Bosi mpya wa City Manuel Pellegrini aliamini angeweza kumpata kirahisi kiungo huyo mwenye maujuzi mengi mwenye miaka 21kutoka klabu aliyokua akiifundisha, kabla ya Madrid kuingilia chezo na kuwatoa kapa. (The sun) Ila usisahau kuambia marafiki wa-LIKE A7Entertainment wapate habari za uhakika na michezo. {PicaSsa}
Posted on: Fri, 28 Jun 2013 05:20:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015