Msahafu wa kihistoria ulioandikwa kwa mkono umeonekana katika - TopicsExpress



          

Msahafu wa kihistoria ulioandikwa kwa mkono umeonekana katika msikiti wa zamani ulioko Bodrum katika mji wa bandari wa Mugla, huko nchini Uturuki. Yüksel Kılınçarslan imam wa msikiti mkongwe uliojengwa mwaka 1737 wa Tepecik ulioko Neyzen Tevfik Avenue, umebainika msahafu huo una umri wa miaka 1200, na uligunduliwa katika chumba cha imamu katika msikiti huo wa zamani ulioko Bodrum. Msahafu huo umekabidhiwa idara ya makumbusho ya mji wa Bodrum. Msahafu huo utapelekwa maktaba ya mji wa İzmir baada ya kufanyiwa baadhi ya matengenezo.Imam Kılınçarslan alisema kwamba uligunduliwa msahafu huo ukiwa umezungushiwa kitambaa. “hatukutoa umuhimu wowote kwamba ilikuwa ni Qurani tunayoijua, lakini nikagundua kuwa ni Qurani iliyoandikwa kwa mkono." Utafiti uliofanywa na wanahistoria kuhusu msahafu huo unaonesha kwamba ni wa miaka 1000 iliyopita. “Nilikwenda Ankara kuzungumza na viongozi na walinambia niutoe kwa taasisi husika,” alisema Imam. Msahafu huo ulioandikwa mkono umepatikana katika msikiti huko Aegean ambako kuna misikiti mingi iliyojengwa tangu kipindi cha utawala wa Khalifa sayyidna Uthman bin Afan Aidha msahafu huo umepatikana na baadhi ya vitabu vya tafsiri ya Qurani.
Posted on: Wed, 18 Sep 2013 14:22:41 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015