¤¤¤NI MIMI NA MOYO WANGU TU¤ Mtunzi: - TopicsExpress



          

¤¤¤NI MIMI NA MOYO WANGU TU¤ Mtunzi: Chicolovebaby Namba:0765,0658, 270133 Sehem:34 Nikiwa nimemkumbatia mama kwa furaha na kumbusu uku nae akiwa na furaha " "Aneth alikua anashangaa tu uku akitabasamu pasipo kusema chochote" "Nae akamsogelea mama nakusalimia" "Shikamoo mama " "Sijambo mkwe wangu mzima mmependeza" "Asante mama mbona mama leo unafuraha sana kuna nini?" "Beibe kumbe nawe umeonae yani nimekuja tu nakuona alivyo na furaha " "Mama mimi ndio napenda uwe nafuraha ivi siku zote " "Ha ha ha kwahiyo hata kama nina njaa niwe nafuraha tu" "Ndio ha ha ha ebu mama niambie eti ni nani kaja hapa nyumbani? " Mmmh hakuna mtu amekuja hapa nyumbani mwanangu kwani kuna tatizo" "Hapana mama dada alinipigia simu akanipa habari fulani ila tuache hayo" "Mchungaji Jacob anakusalimia sana na pia amesema nikupeleke nyumbani" "Napia mama unajua nilizungumza nae kuhusu yale mambo yangu na Mkwe wako ya kwenda kujitambulisha kwao" "Akasemaje sasa ! "Yeye amesema hana tatizo yuko tayari kunipeleka na kujitambulisha kama mzazi wangu" "Basi itakua jambo zuri sana tutazungumza kwa kina zaidi tujue nini tutafanya kabla yakwenda" "Sawa mama vip mgonjwa anaendeleaje saivi? "Mgonjwa hali yake inaendelea vizuri kabisa nilikua hapo tangu Asubuh na mme wake? "Mama mme wake? Umewezaje kukaa nayule shetani mtu anaroho mbaya kama nini" "Hapana mwanangu tumezungumza sana na pia amenitaka radhi kwa kila jambo alilofanyia familia yangu hakika amebadilika sana" "Mama unauhakika gani amebadilika tabia ya mtu ni kama ngozi mama yule mzee ni mtu katili sana hapa duniani" "Nakama mtaendelea kua karibu yake mimi nitaondoka hapa nyumba sitakua weza kua karibu na mtu aliyeniletea matatizo mengi sana ndani ya moyo wangu" "Nikiwa nimeshikwa na hasira machozi yakawa yananitoka nikainuka pale nilipokua nimekaa na mama pamoja na Aneth nataka kuondoka" "Sikiliza mme wangu usiwe na hasira uwezi jua nae moyoni ameumia kiasi gani hadi ametaka kuja kuongea na wewe" "Ile nageuka ivi nataka kwenda ndani nikapumzike na kutana uso kwa uso na Mzee Msiba nae ndio anakuja hapa nyumbani kuzungumza nami" "Nikamtazama kwa hasira umekuja kufanya nini hapa wewe shetani usie kua na huruma na wanadamu" "Kijana wangu usinijibu majibu mabaya hata salamu utaki kunipa unanishambulia kwa maneno makali" "Ndio nakushambulia kwa maneno makali maana wewe sio binadamu na pia siwezi kupa salamu yangu ebu fikiria yale yote uliyonitengea mimi pamoja watu wengine yalikua sahihi" "Kwanza naomba urudi kwako sitaki mazungumzo na katili hata siku moja yale uliyonitendea inatosha" "Siku jua kama wewe mzee ni katili hadi katika familia yako" "Uku machozi yakinitoka aaah! hiii ! Mmmh uuuh mama mimi nitakosa furaha sijui nitaenda wapi mimi uyu mtu na muogopa sana" "Nikiwa nalia kwa hisia kali Aneth akanisogelea na kunikumbatia uku akinibembeleza kama mtoto" "Mama nae akapata uchungu baada yakuona nalia kwa kwikwi" "Baba ulimfanyaje huyu kijana mbona anahasira sana nawewe" "Kipindi chote icho mimi nalia mzee msiba nae alikua kwenye mawazo mazito sana uku akionekana kujutia kile alichofanya" "Taratibu nae akawa anaongea kwa sauti ya huruma uku machozi yakimtoka akashindwa jizuia na kuanza kulia kama mtoto" "Nimejifunza mengi hakika kipindi chote nimekua na nikiishi katika chuki na majirani zangu pamoja na hata familia yangu" "Ila kipindi niko lockapu nimejifunza mengi sana nilimjeruhi mke wangu kipindi chote nilikua sijui nani atamuhudumia ila nilipotoka nilishangaa sana pale nilipo muomba msamaha na kuniambia kama sio mama Alvin angekua amekufa" "Nashukuru sana hii kwa wema wote mliotenda dhidi ya mke wangu na pia namuomba Alvin anisamehe nikweli nilikusudia hadi kumuua kutoka na roho ya chuki iliyokua imepandikizwa ndani ya moyo wangu" "Mzee Msiba akanisogelea na kunipiga magoti" "Nami nikamsogelea taratibu hapana hapana mzee usifanye ivyo mimi ni kijana mdogo sana kwako upaswi kunipigia magoti " "Nikamtaza kama dakika mbili ivi kisha nikamgeukia mama alafu Aneth nikakumwambia!.........ITAENDELEAA! Usikose fuatilia hadith hii Sehem: 35 @Chicolovebaby@
Posted on: Thu, 22 Aug 2013 05:06:58 +0000

Trending Topics



e thank you to everyone who supported
The first day of the New year has come and gone. I have spent this
Knowledge During a recent robbery in Hong Kong, the bank

Recently Viewed Topics




© 2015