[SIZE=4][FONT=book antiqua]Hongera Jenerali Abdel Fattah - TopicsExpress



          

[SIZE=4][FONT=book antiqua]Hongera Jenerali Abdel Fattah al-Sisi(Mkuu wa Majeshi Misri) na wananchi wa Misri kwa kuipindua serikali yao.Siogopi mitazamo ya wenye akili ndogo kuchukulia hili kwa mtazamo wa uhaini(treasonable perception),nipo tayari kwa lolote.Nililalumiwa sana kwenye mitandao ya kijamii kwa kuunga mkono Msimamo wa Jeshi la Misri kusimama na Wananchi.Leo yametimia.Bado naunga mkono na ninalipongeza jeshi la Misri kwa kumpindua Mohammed Morsi.Huu ndiyo mfano bor a wa jeshi linalojiita la wananchi.Sina shaka na uwezo na uzalendo wa jeshi letu la wananchi(JWTZ),natoa wito kwa vijana wote waliotimiza vigezo vya kisheria kujiunga na jeshi waendelee kujiunga kwa wingi……………!!!!!!!Msinihoji,watch this space! Pamoja na kwamba najua marekani haikutaka kuona Morsi anashinda uchaguzi(tulijadili hili kwa kina kule Jamii Forums kwenye Jukwaa la Great thinkers katika Thread ya DURU ZA SIASA by,Nguruvi3)na nilisema kwamba Marekani kupitia shirika la kijasusi la CIA lingemgeuza Morsi kuwa Salvador Allende wa Afrika na zama hizi,lakini bado Morsi aliwapa fursa kupitia makosa yake na ulevi wa madaraka aliouonyesha.Wanamapinduzi wa kweli hawafanyi hivyo.Nilimshangaa sana alipojipendekeza kwa mataifa ya Magharibi na kumponda Rais Bashar Al-Assad wa Syria na kutaka Regime Change.Mnafiki mkubwa,malipo ni hapa hapa duniani. Alisahau kuwa Marekani walitumia jeshi kupitia CIA kumpindua Hugo Chavez kule Venezuela lakini jenerali Morales alituma kikosi cha makomando wa kutisha na ku,muokoa Rais huyo aliyechaguliwa na wananchi.Similar incident appeared in Greece back in 1974 when a CIA instigated military coup overthrew the anti-American prime minister Andreas Papandreou and then the caretaker prime minister Mr. Kanelopoulos. Ikumbukwe mwaka 2011 Wananchi wa Misri walimiminika katika viwanja vya Tahrir Square kutaka Rais Hosni Mubarak (kibaraka wa Marekani ) aondoke madarakani na baadaye katika matunda ya mapinduzi yale Uchaguzi ulifanyika na Mohammed Morsi wa Chama cha FJP(Freedom and Justice Party) ambacho hapo kabla kilikua chama cha kundi lenye msimamo mkali la Muslim Brotherhood akachaguliwa kuwa Rais mbele ya mgombea aliyekua akiungwa na Jeshi lakini pia alisadikika kuwa kibaraka wa Mubarak kwa kuwa alikua mkuu wake wa idara ya usalama.Chama Cha Muslim Brotherhood nilikua nikikiunga Mkono sana hasa watu kama El-Baradei(aliyekua mkuu wa shirika la kudhibiti niuvu za atomiki duniani) walipokuwa wakisimama katika majukwaa ya kimataifa na kujenga hoja.Mohammed Morsi hajatimiza matakwa ya umma,wananchi wameingia barabarani na kutaka mabadiliko ila yeye kwa jeuri akaendeleza ubabe.Jeshi limeamua kusimama na wananchi maana jeshi lilimpa masaa 48 awe amesikiliza matakwa ya wananchi na muda huo ulifika mwisho leo mida ya sa 10:35 jioni hivyo jeshi likaamua kuteka maeneo muhimu ikiwemo televisheni na redio ya taifa.Hili ndiyo aina ya Jeshi ambalo hata mimi katika maisha yangu nitatamani kuwa amiri jeshi mkuu wake. Haya ni mapinduzi ya kipekee Afrika,tumepiga hatua moja kubwa zaidi.Ukiniambia nichague kati ya demokrasia ya kizuzu na mapinduzi ya kijeshi,always my option ni military takeover.Nina special passion na jeshi Umoja wa Afrika wana tabia chafu ya unafiki kwa kuwa ni club ya madikteta tu,utasikia wanakurupuka kama chafya kutaka kuitenga Misri na kutaka kujenga hoja kwamba katiba haijazingatiwa,huo ni upuuzi maana katiba inatokana na wananchi ambao waliingia mitaani na jeshi likawaaunga mkono hata mimi ipo siku kama uonevu na ukandamizaji hapa Tanzania utaaendelea hivi name nitazidi kusukuma wananchi wadai haki zao kwa njia hii.Nimefurahi kuona mkuu wa majeshi wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ameasema pamoja na suspension ya constitution lakini serikali ya mpito itaongozwa na Jaji mkuu wa mahakama ya juu.Huu ni uamuzi wa Busara nauunga mkono Bernard Membe,haraka sana anatakiwa kuitambua serikali mpya ya misri na aache sera za kivivu za kuegemea msimamo wa AU(club ya madikteta ambao siku zao zinahesabika). Mwezi March mwaka huu ilikua zamu ya Jamhuri ya afrika ya kati ambako Waasi wa kundi la SELEKA walichukua serikali dhidi ya mafisadi na walevi wa madaraka,niliwaunga mkono na nitaendelea kuwaunga mkono wanaosimama na wananchi hadi siku yangu/yetu itakapofika kuongoza mapinduzi. Goodbye Morsi. One can blame Americans as some of us are doing here. But as they say, devil can’t enter until we lay out a way for it to enter. Morsi should have paid greater heed to the concerns of protesting Opposition groups, liberal sections and various sectarian minorities (Muslim and Non-Muslims) of Egypt. Democracy and Tyranny of electoral majority are not one and the same thing……..
Posted on: Thu, 04 Jul 2013 04:42:20 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015