"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba - TopicsExpress



          

"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba xxii Hatimaye nilifikishwa tena kituoni na kuwekwa sero kwa mara ya pili "Sijui dada Magreth alifanikiwa kupata ule mkopo?"Nilijiuliza nikiwa ndani ya sero "Ngoja mama akija nimuombe tu akamuangalie dada Magreth"Niliwaza huku nikijilaumu kwenda kwa kina Anitha badala ya kwenda ofisini kwa dada Magreth!! Siku ile nililala sero,,mbu,,kunguni na chawa vilinitesa usiku kucha,,sikupata ata lepe la usingizi,,usiku ulikuwa mrefu sana kwangu tofauti na siku nyingine,,hatimaye ilifika asubuhi "Kijana jiandae kwenda mahakamani"Afande mmoja alikuja kuniambia,,lisaa limoja baadaye mimi na baadhi ya wafungwa wenzangu wengine tulikuwa ndani ya karandinga kwa ajili ya kufikishwa mahakani "Kwakweli nna kila sababu ya kwenda jela"Niliwaza nikiwa ndani ya gari lile la mapolisi "Sijui kwanin huyu mrembo Anitha amenikaa kiasi hiki akilini"Niliendelea kuwaza mambo mengi sana kuhusu Anitha,,hatimaye tulifika mahakamani,,mmoja badala ya mwingine alianza kwenda kizimbani kila iliposomwa kesi yake Mda wote moyo wangu ulikuwa ukinienda mbio,,nilijua fika maisha yangu yote yangekuwa ya gerezani kwani sikuwa na ndugu ata mmoja wa kuweza kunilipia deni lile nililokuwa nikidaiwa Nilishangaa hadi muda unaish jina langu halikutajwa kabisa katika watu waliokuwa wakisomewa mashtaka yao pale mahakani...... "Kijana nenda tu pale kwa ndugu zako wanataka walimalize swala lako"Askari mmoja aliniambia wakati nikijiandaa kurudi kwenye karandinga Nilifurahi sana,,haraka nikaanza kutembea kuelekea walipokuwa wamesimama ndugu zangu,,ndugu wengi sana walijitokeza mahakamani pale "Shikamooni..........."Niliwasalimia wakubwa wangu wote niliowakuta pale,,kila mmoja aliitikia lakini mama alionekana kuwa mnyonge kupita kiasi nikajua fika alikuwa amekasirika "Pole kwa matatizo kijana.........."Baba yangu mkubwa aliniambia huku akiniangalia usoni "Asante baba........."Niliitikia huku nikimuangalia mzee yule aliyekuwa na busara sana "Baba haya matatizo yako tumeyasikia kwa muda mrefu sana ila kwa hapa yalipofika lazima tuyaingilie kati"Baba mkubwa aliongea huku akiniangalia usoni "Hapa unavyotuona tumechangishana wote imepatikana hii laki tano na elfu hamsini"Mzee yule aliongea huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha hela alizozitaja "Tunaomba utangulize kwanza hii hela kwa muhusika na umueleze kuwa atuvumilie ndani ya wiki hii tutammalizia mzigo wake"Baba mkubwa aliongea huku akinikabidhi kiasi kile cha hela nami haraka nikakipokea "Shemeji naomba chukua hizo hela twende nazo moja kwa moja kwa anayemdai"Mama alimwambia baba mkubwa "Mwanao akili zake sio nzuri,,juzi juzi tu amepewa laki mbili na elfu hamsini na dada yangu ili apunguze deni lakini sijui ata kazipeleka wapi......."Mama alimwambia baba mkubwa,,wote wakashangaa,,mala ghafla Magreth alifika tulipokuwa tumesimama "Wilbat ndo umefanya nini sasa........?"Magreth aliniuliza kwa sauti ya kunishangaa "Au hukuwa na shida hela ulikuwa unapima imani yangu?"Magreth aliniuliza huku akiniangalia vizuri Kwakweli sikuwa na la kumjibu Magreth,,ndugu zangu wote wakawa wanamshangaa Magreth aliyeonekana kuwa na huruma sana juu yangu "Dada kwani vipi.........?"Shangazi yangu alimuuliza Magreth na bila kusita Magreth akawaeleza kila kitu "Wifi nahisi huyu mwanao ana matatizo ya akili........"Shangazi aliongea huku akimuangalia mama yangu "Na ndomana nimeomba hizo hela tuzipeleke wenyewe na sio yeye"Mama aliongea huku akiniangalia kwa hasira "Ilikuwa tupate hela zote leo mapema sana ila wameshindwa kunipa sababu mtu aliyetakiwa kupewa ambaye ndo Wilbat hajaja kabisa ofisini"Magreth aliwaambia ndugu zangu,,kila mmoja aliniona mjinga "Namimi wacha niongezee hii laki tatu na elfu hamsini"Magreth aliongea huku akitoa hela kwenye mkoba wake na kumkabidhi mama yangu aliyekuwa ameshika na zile hela nyingine jumla ikawa laki nane "Tena kuna nafasi za kazi kama yupo tayari kesho atume maombi ya kazi ili hilo deni lililobakia alipe mwenyewe"Magreth aliongea kwakweli kila mmoja alimsifia Magreth kwa moyo wake wa kujitolea juu yangu!! ************** "Tajiri wako ametuelewa ila amesema ndani ya wiki mbili lazima hela yake iliyobakia iwe imeshapelekwa"Mama aliniambia aliporudi nyumbani usiku "Pia sitaki kuona wala kusikia habari zozote na huyo mwanamke wako anayekufanya upate uchizi bado mtoto mdogo"Mama aliniambia kisha akainuka na kuelekea chumbani akiniacha na mawazo kichwani "Nani anayemwambia mama habari zote hizi..........?"Nilijiuliza huku nikianza kupatwa na hasira "Lazima kuna mtu atakuwa anacheza na akil zangu........"Niliendelea kuwaza kisha haraka nikakumbuka kuwa nina barua ya kuandika kwa ajil ya maombi ya kazi "Loooh Anitha wangu jamani........"Ghafla mawazo ya Anitha yakanijia tena kichwani.........!! ********* Itaendelea................. Naomba Niwatakieni Usomaji Mwema Wa Simulizi Hii Na Niwatakieni Siku Njema #REVENGE Inakusubiri Kwa Hamu Msomaji Wangu By #Hajrat
Posted on: Tue, 10 Sep 2013 21:50:02 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015