"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba - TopicsExpress



          

"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba xxx Hatimaye kidume nikawa mfanyakazi rasmi wa shirika lile kwani nilishatambulishwa kwa wafanya kazi wenzangu kuwa mi ndo muhasibu wa shirika basi asilimia kubwa ya wafanyakazi wakawa wananiita bosi "Bosi nimekuja nna shida ya kukusalimia tu.........."Magreth alinitania alipoingia ofisini kwangu "Hakuna shida unaweza kunisalimia"Nami niliitikia kiutani huku nikitabasamu "Kwakweli Magreth nashukuru sana kwa msaada wako....."Nilitumia nafasi ile kutoa shukrani zangu kwa Magreth "Aaah jamani Wilbat,,usijari kabisa mana hayo ni mambo ya kawaida"Mgreth aliongea huku akitabasamu "Maisha ni safar ndefu sana hivyo basi naamini ipo siku na wewe utakuja nisaidia"Magreth aliongea huku akimuangalia Wilbat usoni,,kwakweli Magreth alionyesha wazi kumpenda sana Wilbat licha ya kujua fika kama Wilbat amenasa kwa Anitha mwanamke aliyekuwa akimsababishia matatizo kila siku!! *********** Wiki ya kwanza iliisha nikiwa kazini,,ikaaja wiki ya pili hatimay ikafika wiki ya tatu nikiendelea kufurahia maisha yangu ya kazi,,kwakweli mwili wangu ulianza kuwa na mabadiliko kiafya kwa yoyote aliyeniona siku za nyuma lazima angetambua wazi kwamba kwa sasa maisha yangu yapo juu ya mstari Nilijitahidi kuhakikisha nakuwa tegemezi sana kwa mama yangu,,yani kila kitu cha nyumbani kilinihusu mimi kuanzia kula mpaka mavazi ya mama yangu sio siri kazi ile iliniwezesha kuingiza kipato kikubwa sana mbali ya mshahara niliyokuwa napokea kwa kila mwezi "Beb kwakweli siku hizi unanawiri sana embu nipe siri ya mafanikio yako"Siku moja Anitha aliniuliza nilipomtembelea nyumbani kwao siku ya jumapili "Aaaah nimeridhika tu na umasikini wangu"Nilimjibu Anitha huku nikitabasamu "Enheee kweli Tanzania kwa sasa ina maendeleo......."Anitha aliongea huku akitabasamu "Yani masikini anatembelea Rav 4 mayai kama hii"Anitha aliniambia akiwa hajaliamini kabisa jibu nililompa "Beb gari ya watu hii nimepewa tu,,si unajua nafahamiana na madereva wengi hapa mjini"Niliendelea kumdanganya Anitha sababu sikuhitaji ajue kabisa kama nimepata kazi iliyobadilisha maisha yangu japo alihisi kitu kama hiko sababu siku zote mwenye pesa huwa anatambulika tu "Vip masomo mpenz wangu......."Nilimuuliza Anitha wangu "Aaaah hivyohivyo tu,,afadhali miezi ifike nifanye mtihani nimalize mana nahisi nimeshachoka na kusoma"Anitha alinijibu "Jitahidi ufahulu mpenz wangu,mana maisha ya mtaani magumu sana"Nilimwambia Anitha "Sawa mpenz wangu nitajitahidi...."Anitha alinijibu Tuliongea mambo mengi sana na Anitha,,lakini kubwa zaidi Anitha aliniahidi jumapili tungekutana kwa ajili ya kwenda kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza nami nikamkubalia hakika nililifurahia sana jambo hilo!! Siku zilienda taratibu sana,,kidume nikajipanga kisawa sawa kuhakikisha siku ya ahadi mambo yanakwenda kama yalivyopangwa,,siku mbili kabla ya siku yetu ya ahadi niliamua kuingia dukani kwa ajili ya kumfanyia shoping ndogo mpenz wangu Anitha Nakumbuka nilimnunulia Anitha simu nzuri ya kisasa,,viatu vya warembo wa kisasa na ata sketi fupi nilizokuwa napenda mwanamke azivae,,nilimnunulia saa nzuri na nguo nyingi za ndani yani tait na chupi za kutosha "Naamini atazifurahia sana zawadi hizi......."Niliwaza nilipomaliza kununua vitu vile!! *********** "Hallow beb wangu za kushinda......."Usiku wa jumamosi niliongea na Anitha kwenye simu "Safi tu mpenzi wangu,,pole na kazi....."Anitha aliniuliza kwa sauti iliyoonyesha wazi kuwa amechoka "Nzuri tu,,enheee lete stori......."Nilimwambia Anitha wangu wakati nipo kitandani nimejilaza "Aaah sina kwakweli zaidi ya uchovu tu"Anitha aliniambia kitu nilichokuwa nimekigundua tangu nianze kuongea naye "Basi pumzika beb wangu ili kesho uwahi kuamka kwa ajil ya kujiandaa"Nilimwambia Anitha "Sawa beb nashukuru........."Anitha aliongea kisha akakata simu jambo ambalo lilianza kunipa mashaka na hofu kubwa moyoni!! Asubuhi ya jumapili niliwahi sana kuamka kwa ajili ya kufanya usafi wa nguo zangu pamoja na kupiga deki chumbani kwangu,,nilipomaliza nilikunywa chai niliyoandaliwa na mama yangu huku nikimpigia simu Anitha aliyekuwa hapatikani kabisa "Sijui ana matatizo gani..........?"Nilijiuliza mwenyewe bila kupata majibu "Au simu yake itakuwa imeisha chaji mana n huu mgao wa umeme wa hapa Jijini"Nilijifariji huku nikiendelea kupiga simu bila kuchoka. Hatimaye nikaona ni bora tu nijiandae niende kwao ili kujua kama mpenzi wangu yupo salama au laa Baada ya kujiandaa nikaingia ndani ya gari yangu na safari ya kwenda kwao ikaanza nikiwa na shahuku kubwa ya kumuona Anitha wangu aliyeniahidi kitu kizuri siku ile ya jumapili.......!! *********** Itaendelea............ R E V E N G E watu wameshaanza kuisoma,,hivyo basi ikiwa bado hujaisoma HAKIKA KIFO NI HAKI YANGU naomba uanze sasa ili tu usome na muendelezo wake Mapenzi ya dhati pia inaendelea kupatikana kwa ambayo hajaisoma kabisa!! Nawatakieni Kazi Njema Siku Ya leo By #Hajrat
Posted on: Mon, 30 Sep 2013 06:14:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015