.....tunaendelea na stori yetu....nilipokuwa nimejilaza pale kitandani nikiwa nimejawa na uchovu kutokana na shughuri niliyoifanya usiku kucha nikajikuta nazama ndani ya usingizi mzito...tukumbuke kuwa muda wote ule mlango ulikuwa wazi baada ya yule mama kutoka alfajir nilishindwa kuufunga kutoka na uchovu pamoja na usingizi ulokuwa ukininyemelea...nikiwa ndani ya usingizi nikahisi kifua kinabana mpaka nikahisi nashindwa kupumua nishtuka kutoka usingizini na kugundua kuwa mwili mzima umelowa jasho mara mbavu zikaanza kunibana nikiwa natapatapa pale kitandani na kila nilipo jaribu kupiga kelele za kuomba msahada kutokana na maumivu makali nilokuwa nikiyasia sauti iligoma kutoka mara ghafla nikasikia sauti ikiangua kilio kutokea juu ya dali huku ikisema "Zungu umenisaliti...umewezaje kulala na mchawi wakati unajua uhasimu wetu na sisi majini sasa utajuta!!"mara ghafla nikasikia vishindo mithiri ya watu wanaangushana mieleka kukulukakala mara nikaona vitu vinaanguka anguka kwambali nikaanza kusikia sauti za mabishano makubwa....kama unataka iendelee SHARE au LIKE
Posted on: Sat, 31 Aug 2013 11:40:19 +0000