1.Watu walipoona mwanamke tasa ndani ya Sarah, Mungu alimwona mama - TopicsExpress



          

1.Watu walipoona mwanamke tasa ndani ya Sarah, Mungu alimwona mama wa Taifa kubwa. 2.Watu walipoona mchungaji mdogo, dhalili ndani ya Daudi, Mungu alimwona Mfalme shupavu wa Israel. 3.Watu walipoona mfungwa duni ndani ya Yosefu, Mungu alimwona Waziri Mkuu mstahiki wa Misri. 4.Watu walipoona mtoto maskini ndani ya Musa, Mungu alimwona Kiongozi mkuu, mwaminifu wa Israel. Hivyo basi, usijali kwamba watu wanaona nini ndani yako, ila machoni mwa Mungu anakuona mtu muhimu sana na ana mipango mizuri juu yako katika kukupatia maisha angavu mbele yako. "YER 29:11-14" Mungu akubariki na kukufadhili "HES 6:24-26"
Posted on: Sun, 21 Jul 2013 06:15:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015