10/10/---- Tarehe kumi mwezi wa kumi miaka iliopita ilikuwa - TopicsExpress



          

10/10/---- Tarehe kumi mwezi wa kumi miaka iliopita ilikuwa maarufu kama Siku Kuu ya Moi. Baada ya Katiba kubadilishwa, sasa ni siku kawaida kama siku zinginezo. Lakini mwenyeji wa siku hii hajawahi sahau siku hii kwani ni muhimu kwake kama tarehe aliapishwa rasmi kama rais wa pili wa Jamhuri ya Kenya. Kwa kawaida yeye hutembele watoto mayatima, wasijiweza, na wengi waliopungikiwa kwa maisha. Ni miaka kumi na moja tangu astaafu kuwa rais wa Kenya lakini angali anasikika na mawaidha yake hutumika mara kwa mara. Jee, umuhimu wa siku hii ilikuwa nini? Jibu unalo. Tarehe 20/10/2013 tunatarajia kuona mengi hasa kwa mashujaa wa tabaka mbalimbali. Westgate mashujaa, wanariadha mashujaa, akina mama mashujaa, vijana mashujaa na viongozi mashujaa sio tu wanasiasa na watu wanaosifika. Shujaa ni mtu yeyeto aliyefanya jambo la maana kuokoa, kuinua au kuletea nchi sifa kwa kuhatarisha maisha yake kwa niaba ya wengi wengi. Kongole mashujaa wetu wa Westgate, dunia inawapongeza sana tena sana!!!!!!!
Posted on: Wed, 09 Oct 2013 14:11:50 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015