A DAY TOO LONG SEHEMU YA 15 Ilipoishia “Sikuamini. Sikuamini - TopicsExpress



          

A DAY TOO LONG SEHEMU YA 15 Ilipoishia “Sikuamini. Sikuamini hata kidogo, huo utakuwa mchezo mchafu mnaotaka kutufanyia” Rais Kyomo alisikika simuni. “Ndio ukweli. Nilimtuma waziri wa Afya kwenda kumchukua chuo ili tumsafirishe lakini akakuta Wamarekani wamemchukua” Rais Ranjit alimwambia . “Huo ni mchezo tu. TUNAMTAKA ABUU WETU” Iliskika sauti ya rais Kyomo na kisha kukata simu. Songa nayo sasa…. Dokta Mickey alikuwa na presha ya kufika nchini Marekani na kueleza kile ambacho alikuwa amekiona nchini India. Moyo wake ulikuwa kama umebeba mzigo mzito, mzigo ambao alitamani kuushusha katika kipindi ambacho angefika nchini Marekani. Muda wote uso wake ulionekana kuwa na furaha kupita kawaida kwa kuona kwamba wakati wa kulipatia sifa zaidi taifa lake la Marekani ulikuwa umefika. Muda wote alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Mara baada ya ndege kushuka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Baltimore, au Washington kama ulivyokuwa ukijulikana Dokta Mickey pamoja na abiria wengine wakateremka kutoka katika ndege ile na kisha kuanza kupiga hatua kulifuata jengo la uwanja huo na kuanza kuchukua mabegi yao ambayo yalikuwa yamekwishachunguzwa na kuondoka mahali hapo. Alipofika nje ya jengo la uwanja wa ndege ule, akakodi teksi na kisha kumwambia dereva ampeleke West Mall, sehemu ambayo ilikuwa ikipatikana Ikulu ya Marekani. Japokuwa dereva alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kawaida lakini dokta Mickey akamuona kama akiendesha kwa mwendo wa taratibu jambo ambalo kila wakati alikuwa akimsisitizia mara kwa mara kwamba aendeshe kwa kasi zaidi. Hapo ndipo alipokumbuka kitu, akaichukua simu yake na kisha kuiwasha na kuanza kupiga namba za rais wa Marekani, Obama na kuanza kuongea nae kwamba alikuwa na jambo muhimu sana ambalo alikuwa akitaka kumwambia kwa wakati huo. Aliongea nae kwa dakika kadhaa na hivyo rais kumtaka kufika katika Ikulu ile kwa ajili ya mazungumzo zaidi kwa kile ambacho alikuwa amemuelezea kwa kifupi. Mara baada ya kufika umbali wa kilometa moja kabla ya kulifikia geti la kuingilia eneo la Ikulu, dereva akasimamisha gari na kisha Dokta Mickey kuteremka na polisi kadhaa kumfuata na kisha kujitambulisha kwao. Kutokana na rais kutoa taarifa za haraka haraka juu ya dokta huyo, akaruhusiwa kuingia ndani ya eneo la Ikulu ile na kisha kuanza kupiga hatua kulifuata jengo lile huku kila kona kukionekana kuwa na kamera pamoja na polisi kadhaa. “Just tell me about it (Hebu niambie kuhusu hilo jambo)” Rais Obama alimwambia dokta Mickey. “I saw a young man (Nimemuona kijana)” Dokta Mickey alimwambia rais. “Which boy? (Kijana yupi?) Hapo hapo Dokta Mickey akaanza kuelezea kile ambacho kilikuwa kimetokea nchini India juu ya kijana ambaye alikuwa ameonyeshewa pamoja na dawa ya kansa ambayo alikuwa ameitengeneza kijana yule, Abuu. Muda wote rais Obama alikuwa ametegesha masikio akimsikiliza Dokta Mickey ambaye alikuwa akiongea huku akiwa haamini kama kweli kile ambacho alikuwa amekiona nchini India kilikuwa kweli. Maongezi yao yalichukua dakika thelathini na ndipo ambapo Dokta Mickey akaamua kuwasiliana na Bwana Thomas, mtu ambaye alikuwa bosi mkuu wa shirika la upelelezi la F.B.I. Maneno ambayo aliongea Dokta Mickey tayari yalikuwa yamemchanganya kupita kawaida, hakuamini kama duniani kungekuwa na mtu ambaye angeweza kutengeneza dawa ya magonjwa ya kansa. Aliongea na Bwana Thomas kwa muda wa dakika moja tu na kumtaka kuelekea katika Ikulu ile kwa maongezi kadhaa. Muda wote rais Obama alionekana kuwa na furaha, tayari aliziona sifa nyingi zikianza kumiminika katika nchi ya Marekani, aliamini kabisa kama angeweza kufanikisha kumleta kijana huyo, Abuu ndani ya nchi yake basi kusingekuwa na ugumu wa kukipigania kiti cha urais kwa chama chake kushinda katika uchaguzi ujao, kwani kile kingeonekana kuwa sababu. “We have to kidnap him, How do you see that? (Inatubidi tumteke. Unalionaje hilo?)” Rais Obama aliuliza. “Good idea (Wazo zuri)” Dokta Mickey alisema huku wote nyuso zao zikiwa zimetawaliwa na tabasamu. Ndani ya dakika ishirini, Bwana Thom akawa amekwishaingia ndani ya Ikulu hiyo na moja kwa moja kukutana na rais pamoja na Dokta Mickey na kisha kuanza kuelezwa kile ambacho kilitakiwa kufanyika katika muda huo. Kilichoelezwa ni kwamba Abuu alitakiwa kuchukuliwa kutoka nchini India na kuletwa nchini Marekani kisiri, na hakukuwa na watu ambao wangeweza kufanya hivyo zaidi ya FBI ambao walikuwa na uwezo mkubwa sana katika mambo mengi hasa utekaji. Hilo likaonekana kuwa wazo zuri ambalo liliungwa mkono na kila mtu, Abuu ndiye ambaye alikuwa akihitajika nchini Marekani kwa wakati huo na ilikuwa ni lazima kutekwa kwani bila kufanya hivyo, Waindi wasingekubali mtu huyo aondoke mikononi mwao. “We are doing this for Americans (Tunafanya hili kwa ajili ya Wamarekani)” Rais Obama alisema huku akiinyanyua glasi yake iliyokuwa na pombe hewani. “For Americans (Kwa ajili ya Wamarekani)” Dokta Mickey na Bwana Thomas walisema. **** Wapelelezi watatu, Jackson, Brian na Shedrack ndio ambao wakaandaliwa kwa ajili ya kufanya kazi moja kubwa ambayo ilikuwa mbele yao, kuhakikisha kwamba kijana Abuu analetwa nchini Marekani kwa njia ambazo wala hazikuwa za uhalali hata kidogo. Kazi ile hasa kwa wapelelezi wale ikaonekana kuwa rahisi sana ambayo wala haikuonekana kuwa na ugumu wowote ile. Walichokifanya ni kujiandaa na kisha baada ya siku mbili kuanza safari huku wakiwa na vifaa vyote ambavyo waliona kwamba wangevitumia katika utekaji huo. Saa saba mchana, ndege ya shirika la ndege la Alliance Airways ilikuwa ikitua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mumbai ambapo wapelelezi wale wakateremka na kisha kuanza kuelekea katika jengo la uwanjani pale huku wakitangulizana pamoja na abiria wengine ambao walikuwa wamefika nchini hapo kwa kutumia ndege hiyo. Wakatoka katika jengo lile na kisha kuelekea nje ambapo wakakodi teksi na kutaka wapelekwe katika hoteli kubwa na ya nyota tano na kisha dereva kuanza kuwapeleka katika hoteli ya Dhabi ambayo ilikuwa katikati ya jiji la Mumbai. Kila mmoja macho yake yalikuwa yakiwaangalia watu ambao walikuwa wakipita huku na kule na huku wengine wakiwa wanaabudu masanamu ya Buddha ambayo yalikuwa yakionekana kuwa kama mungu wao mkubwa katika nchi hiyo. Baada ya dakika ishirini, teksi ile ikasimama nje ya hoteli ya Dhabi na kisha kuanza kuelekea katika sehemu ya mapokezi na kuchukua vyumba vitatu na kuanza kuelekea huko. Kwa wakati huo, kila mmoja alikuwa akifikiria kazi ambayo ilikuwepo mbele yao, kazi ile wala haikuonekana kuwa kubwa, walitegemea kuifanya bila kugundulika na mtu yeyote yule. Mara baada ya kuweka mabegi yao katika vyumba vya, wakakutana katika chumba cha Shedrack na kisha kutoa ramani kubwa ya dunia na kisha kuanza kuangalia nchi ya India. Kitu cha kwanza walichokifanya mahali hapo ni kuangalia ramani nzima ya India na kisha kuangalia mipaka na sehemu nyingine. “Tukimteka, tutaanza kuelekea Bhopal ambapo tutatumia mwendo wa saa moja. Tukifika hapo, tutaendelea na safari yetu ya kuelekea Guna. Kwa sababu tukifika huko kutakuwa tayari ni jioni, hivyo tutaendelea na safari yetu kidogo na kuelekea Udaipul. Tukifanikiwa kufika hapo, tutalala na kisha kesho yake asubuhi na mapema kuanza safari ya kuelekea Jaisalmer ambapo kupitia mpaka huo tutafanikiwa kuingia katika nchi ya Pakistan” Shedrack aliwaambia wenzake huku akiwaonyeshea ramani ile. “Ni mwendo gani kutoka hapa mpaka Jaisalmer?” Jackson aliuliza. “Ni mwendo wa siku moja mbili. Ila kwa sababu mimi ndiye nitakuwa dereva, tutatumia siku moja na nusu” Shedrack aliwaambia. “Mmh! Tutafanikiwa kufika muda muafaka?” “Sana tu. Hilo wala hautakiwi kuhofia kabisa” “Sawa. Baada ya hapo nini kitaendelea? Unafikiri mpakani tutaruhusiwa kuvuka pamoja nae?” Brian aliuliza. “Hilo si tatizo kabisa. Tukifika hapo, tunatelekeza gari na kisha kuanza kuingia porini, tutatumia njia za porini tu” Shedrack aliwaambia. “Mbona naona zoezi kama litakuwa gumu” “Hapana. Sio zoezi humu kabisa. Hili ni zoezi rahisi sana. Au unavyofikiri ugumu wake upo wapi?” Shedrack aliuliza. “Porini” “Kumbuka kwamba tuna bunduki” “Sawa” “Sasa tatizo lipo wapi?” “Huyu mtu ataweza kwenda na sisi kwa mwendo tunaoutaka na wakati nimesikia kwamba ni kilema?” “Usijali. Hata kubebwa atabebwa ili mladi afike salama” “Sawa. Hapo nimekuelewa. Ila bado nina swali” Jackson alimwambia Shedrack. “Swali gani tena?” “Tukifika Pakistan, nini kitaendelea? Au tutakwenda mpaka Karachi?” “Hapana. Karachi ni mbali sana. Kama tungetaka kutumia boti basi tungekwenda huko” Shedrack alimjibu. “Sasa tutaelekea wapi? Islamabad?” “Napo mbali sana. Kama tungekuwa tunataka kuelekea Afighanistan tungekwenda Islamabad” “Sasa sisi tutapitia wapi?” “Hapa tutaelekea Raymar na kisha kuchukua ndege ya kivita itakayokuwa kwenye kambi ya Kimarekani iliyokuwa hapo” “Mmmh! Lakini kabla ya kufika hapo si itatubidi tupitie Sukkur, sehemu yenye wanajeshi wa kigaidi wa kundi la Maashi?” “Hatutopitia huko. Tutachukua njia mojawapo ambayo inapita porini sana na kutokea Raymar. Usijali. Tutafika salama na mtu wetu” Shedrack alimwambia. “Kama ni hivyo, sawa” Mipango yote ilitakiwa kupangwa katika mchana huo, walikaa na kupanga mpaka namna ya kupata gari ambapo wangemtumia mtu yeyote kuwakodishia gari na kisha kulitumia katika kazi yao. Hawakuwa na tatizo la fedha, serikali ya Marekani ilikuwa imetoa kiasi kikubwa sana kwa ajili yao, kilichotakiwa ni kufanyika kwa kazi ambayo ilitakiwa kufanyika.. Siku hiyo hiyo wakaamua kumtafuta kijana mmoja ambaye alikuwa tayari kuingiza kiasi cha dola elfu saba kwa kukodisha gari tu. Wala hawakupta tabu kumpata kijana huyo ambaye moja kwa moja akaelekea katika sehemu za kukodisha magari na kuchukua gari moja na kwenda nalo na kuwagawia huku wakiahidi kumrudishia baada ya saa sita. Usiku wa siku hiyo wakaamua kuhama hoteli na kuhamia katika hoteli nyingine ambayo ilikuwa pembezoni kidogo mwa jiji la Mumbai ili kuepuka usumbufu kutoka kwa kijana ambaye walikuwa wamemtumia kwa ajili ya kukodisha gari lile. “Tusipofanikiwa kumteka mtu huyu, nitaacha kazi” Mpelelezi Shedrack alisema huku akiwa na uhakika wa kumteka Abuu ambaye kwa wakati huo alionekana kuwa lulu duniani. ********************* ****** Je nini kitaendelea hapo..??
Posted on: Mon, 19 Aug 2013 05:26:58 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015