Asalamu Aleikum ndungu zangu waki islam na waomba niwasimulie hiki - TopicsExpress



          

Asalamu Aleikum ndungu zangu waki islam na waomba niwasimulie hiki kiswa nanyie mutafakari. Kuna bwana mmoja alikua shambani kwake akilima kwa bahati nzuri alipokua akichimba chimba akapata almasi kubwa sana akamua kwenda mjini kuiuza alipomuonyesha sonara hio almasi yule sonara akamwambia yule bwana kua hio almasi niya thamani kubwa sana na yeye hakua na uwezo wakuinunua. lakini akampeleka kwa mfalme mfalme kuiona hio almasi yenye thamani isio julikana akamua kuinunua mfalme akawaamrisha washika hazina zake kesho mutamfungulia huyu bwana bohari zangu za mali kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni achukue anachotaka yule bwana usiku huo hakulala kwa kuaaza atachukua nini asubuhi saa 12 akafunguliwa bohari yule bwana akaingia ndani katika kuangalia angalia achukue nini akaona kitanda cha dhahabu kwa vile alikuapeke yake ndani akamua alale kidogo kwenye kitanda cha dhahabu yule bwana akachukuliwa na usingizi ilipofika saa 12 jioni mueka hazina akaja kufunga bohari ikabidi wamuamshe yule bwana atoke nje jamaa akatoka patupu. Ndungu zangu kiswa hichi ni mfano wa ramadhani ramadhani ni kama almasi yenye thamani kubwa sana thamani isio julikana kwa hio twakumbushana tusiwe kama huyu bwana tukalala tuchukuwe fursa hii tuchume tunavyo weze katika mwezi mtukufu huu unaokuja wa ramadhan. Ujumbe huu nawaomba muwatumie ndugu na marafiki munao wapenda Wabillahi taufiq
Posted on: Wed, 26 Jun 2013 16:53:55 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015