Asubuhi maridadi hali ya hewa ni wastani. Joto na baridi zatoshana - TopicsExpress



          

Asubuhi maridadi hali ya hewa ni wastani. Joto na baridi zatoshana baada ya kushuhudia mvua ya rasharasha usiku wa kuamkia leo. Miyale ya jua inaongeza umaridadi kwenye nyasi pale ambapo matone ya mvua yametua waweza dhania ni vioo vimetupwa nyasini lakina apana ni vile miyale ya jua imemulika matone mle nyasini. Nyuni wanaburuka angani wakishukuru Mungu wao. Upepo nao haukubali mawingu kukaa pahali pamoja yanakimbizwa mbio ajabu. Matawi ya miti inapepea utadhani ni mashindano. NAMI SINA LINGINE ILA TU KUMSHUKURU MUUMBA WA VITU HIVI VYOTE MUNGU ALIE ENZINI JUU JUU KABISA.
Posted on: Sat, 23 Nov 2013 06:50:21 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015