BAADHI YA MARAFIKI ZANGU WASIOPUNGUA WATANO WALIWAHI KUKIONA CHA - TopicsExpress



          

BAADHI YA MARAFIKI ZANGU WASIOPUNGUA WATANO WALIWAHI KUKIONA CHA MOTO ENEO HILI.............!!!!! Waijua nchi ndogo ya Lebanoni ndani ya Tanzania? Ama kweli duniani kuna vituko na malimwengu ndio wahanga wa vituko, Magenge ya uhalifu nchini yapo mengi sana, lakini hili la Lebanon limevuja rekodi, Kama huyajui magenge yanayotisha/yenye vituko kwa tanzania hii basi sikia hii, Nenda sasa nyuma ya Ikulu ya Tanzania kuvuka tu barabara ya baharini, kuna mageti hivi, huko kila maasi ya duniani hapa yapo huko, wenyewe wanakuita Lebanon, Wana kiongozi wao na hufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, Huko watu wanaoana na kuzaliana huko huko, tatizo ni kuwa unaweza kukuta geto wameoana kikameroni Wale tai wa ikulu wanaishia kule kule, haiishi wiki lazima wamle mmoja, Kila aina ya pombe inayopatikana Tanzania hapa pia inapatikana huko na kila aina ya madawa ya kulevya yanapatika huko, Mwambieni Mwakyembe kama anajiweza aende akawatoe pale, mtaa ule upo tangu nchi haijapata Uhuru, Wao wanasema hawakutawaliwa na Mjerumani wala Muingereza, Enzi za Mjerumani ilikuwa ndio Bandari yakuingilia Dar kabla ya kuhamishiwa huku St. Joseph, Kila aina ya uchafu wote unaoujua duniani kule utaukuta, Saa nane usiku unaweza kukuta wenzio wanaangalia taarifa ya habari ITV au TBC ya saa mbili usiku, Ukiagiza supu ya utumbo jiandae kuletewa taulo hili la kuogea lililoungwa na nazi safi, utaishia kunywa supu tu nyama huli, na muhudumu anakwambia kuwa usitupe nyama utakayoshindwa kula, kuna kibakuli maalumu cha kuhifadhi tayari kwenda kuungwa kwaajili ya wateja wengine! Aina za pesa zote dola, yen, kwacha, mitikashi, rupia,paund nk zote zinatumika vizuru tu feki na original! Na zaidi kuna swimming pool la kale lililokuwa likitumiwa na mtawala wa kijerumani hivyo kila siku wao wanakula bata tu masaa yote, Hiyo ndio nchi ya Lebanon yenye familia zisizozidi 200 Ukiwa na gari unatoka mjini unataka kuigia feri pale kwenye makutano ya osheni rodi mbele yako kuna mageti makubwa mawili, Sasa geti la kwanza kushoto, ukiingia hapo jua umeingia nchi ya watu, Unaweza uingilia nyuma ya Hospitali ya Osheni Rodi baharini, kuna kamtaa hivi usioeleweka kama mabanda sio mambanda, Nchi hiyo ina uhusiano mzuri wa kidiplomasia ambao ni wakihistoria na nchi nyingine ya Kwazulu iliyopo Kigamboni maeneo ya Sheli ya kwanza unapokwenda Mjimwema, wanachoma Chokaa hivi, eneo hilo lilikuwa kiwanda cha kutengeneza chokaa cha mmoja wa waasisi wa Taifa hili Abdul Syiks miaka ya 1948 huko, Ukitaka kwenda huko simu, pesa nyingi, suti, viatu vizuri achana navyo kabisa, nenda kama baharia unayehitaji bangi na mengineyo, Sio kwamba polisi hawajui, bali baadhi yao ni sehemu ya wakazi wa huko, Au ukiwa na boti zunguka soko la feri
Posted on: Tue, 03 Sep 2013 20:36:38 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015