BARCELONA, HISPANIA KAMA Cesc Fabregas ataenda Manchester United, - TopicsExpress



          

BARCELONA, HISPANIA KAMA Cesc Fabregas ataenda Manchester United, ataungana na baadhi ya wachezaji ambao hawakufikiriwa kucheza katika timu pinzani, lakini wakafanikiwa kujiunga kwa kupitia mlango wa nyuma. Pesa ndio kila kitu. Fabregas alianzia maisha yake ya soka Arsenal na baada ya kurudi nyumbani Hispania, sasa anatajwa kutaka kurudi tena England kucheza kwa mahasimu wa Arsenal, Manchester United. Si yeye pekee, wapo wanasoka wengine waliowahi kutumia njia hii. Peter Schmeichel Haikutazamiwa kama siku moja Schmeicheil angeichezea Manchester City kutokana na kunywa maji ya bendera akiwa na Manchester United, mahasimuwa kufa wa Man City. Hata hivyo, alipoachana na Man United mwaka 1999, alienda zakeSporting Lisbon ya Ureno na kuichezea kwa misimu miwili kabla ya kurudi England na kutuaAston Villa. Misimu miwili baadaye alisajiliwa na mahasimu wakubwa wa United, Man City. Mashabiki wengi walimshangaa lakini hakujali. Schmeichel anashikilia rekodi ya kucheza mechi za watani wa jadi hao bila ya kupoteza akiwa na timu zote mbili katika nyakati tofauti. Akiwa na City walishinda uwanjani kwao, Maine Road na kutoa sare Old Trafford. Paul Ince Akiwa ameichezea Manchester United mechi 206, kocha Alex Ferguson aliamua kumuuza Ince ghafla tu kwenda Inter Milan ya Italia.
Posted on: Fri, 26 Jul 2013 04:09:22 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015