BBC Swahili Katika Amka na BBC asubuhi hii: Mapigano yazuka tena - TopicsExpress



          

BBC Swahili Katika Amka na BBC asubuhi hii: Mapigano yazuka tena kati ya serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23. Na hofu ya mapigano yasababisha mamia ya wakimbizi wa Congo kukimbilia nchini Uganda. Kiasi ya watu 30 wameuawa kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya watu waliojihami kwa bunduki kuushambulia msafara wa harusi. Na Polisi nchini Tanzania imeanza uchunguzi dhidi ya raia watatu wa China waliokamatwa wakiwa na shehena ya pembe za ndovu. Jiunge naye Maryam Dodo Abdalla kwa haya na mengineo mengi muda mfupi ujao, hewani na katika mtandao
Posted on: Mon, 04 Nov 2013 02:35:55 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015