BEI YA MAJI KUPANDA Watumiaji wa huduma za mamlaka ya maji safi - TopicsExpress



          

BEI YA MAJI KUPANDA Watumiaji wa huduma za mamlaka ya maji safi na maji taka Dar es Salaam, DAWASCO, wanatarajia kuendelea kuumizwa na kupanda kwa gharama za maji, kutokana na mamlaka hiyo kuhitaji shilingi Trilioni 1.49 za ukarabati wa miundombinu yake. Mamlaka hiyo, hadi sasa haina vyanzo vya fedha vya kuaminika, hali inayoifanya kutafuta namna mbadala ya kupata fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu iliyoharibika vibaya kutokana na hujuma ama kufanya kazi kwa muda mrefu. DAWASCO imeiomba mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na Nishati, EWURA kupandisha bei ya maji kutoka shilingi1,077 kwa lita hadi shilingi 1,627, ili pamoja na maboresho hayo ikabiliane na changamoto ya upungufu wa maji kwa wateja Milioni 4.5 wanaotumia huduma zake. Uhaba wa vyanzo vya maji, gharama za miradi, uchafuzi wa mazingira pamoja na hujuma za miundombinu zimetajwa kuwa changamoto zinazoikabili sekta ya maji hapa nchini.
Posted on: Thu, 26 Sep 2013 15:23:15 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015