BELHANDA KIKWAZO NJIA YA KWENDA BRAZILI 2014 MCHEZO WA KESHO NA - TopicsExpress



          

BELHANDA KIKWAZO NJIA YA KWENDA BRAZILI 2014 MCHEZO WA KESHO NA MOROCA NI MACHACHE KATIKA SPORTS YA TOP RADIO FM JUNE 7 2013 radiostationstz KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema kwamba, kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji Morocco kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia, anamuhofia sana mshambuliaji wa Simba hao wa Atlasi, Younes Belhanda (23) wa Montpellier ya Ufaransa Akizungumza na Waandishi wa Habari leo asubuhi katika hoteli ya Pullman, Marakech, Poulsen alisema mchezaji huyo ana kila sababu ya kucheza vizuri kesho ili kuzidhihirishia klabu za Ulaya zinazotaka kumng’oa Montpellier kwamba yeye ni bora. “Anatakiwa na Inter Milan, AC Milan, Galatasaray na Aston Villa na dau lake ni Pauni Milioni 20 na klabu yake tayari imekubali kumuuza. Hivyo huyu ni kati ya watu ambao wananifanya niifikirie mechi ya kesho itakuwa ngumu,”alisema. Pamoja na hayo, Poulsen alisema kwamba vijana wake wapo vizuri na wanampa matumaini makubwa kuelekea mchezo huo, ambao amepanga kucheza kwa mfumo wa kushambulia zaidi. Stars, leo jioni itacheza kwenye Uwanja wa Marakech ili kuuzoea kabla ya mtangange huo wa kesho, ambao utaanza Saa 3:00 usiku za hapa, sawa na saa 5:00 usiku za nyumbani Tanzania. Kim amesema lengo ni kushinda kesho ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil. RATIBA YA KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2014 All times CAT (SA, GMT+2) Friday 07 June 2013 Libya v Congo DR Tripoli 17:30 Sudan v Ghana Omdurman 19:00 Saturday 08 June 2013 ... Uganda v Liberia Kampala 15:00 Zambia v Lesotho Ndola 15:00 Botswana v Ethiopia Lobatse 15:00 Central African Republic v South Africa Yaounde 16:00 Gabon v Congo Franceville 16:30 Angola v Senegal Luanda 17:00 Sierra Leone v Tunisia Freetown 18:30 Gambia v Ivory Coast Bakau 18:30 Cape Verde v Equatorial Guinea Praia 19:30 Morocco v Tanzania Marrakech 22:00 Sunday 09 June 2013 Zimbabwe v Egypt Harare 15:00 Niger v Burkina Faso Niambey 17:00 Benin v Algeria Porto Novo 17:00 Togo v Cameroon Lome 17:30 Guinea v Mozambique Conakry 19:00 Mali v Rwanda Bamako 20:00 MADRID- SPAIN. Kocha wa Timu ya taifa ya spain,Vicente Del Bosque amekili kuwa hana mshambuliaji ambaye anaweza kumtegemea katika kikosi chake kwa ssasa mabingwa hao wa dunia humtumia zaidi Cesc Fabrigas kama namba 9 feki na licha ya kuwaita kikosini,Daid Villa,Fernando Torres na Roberto Saldado kw a ajili ya kombe la shirikisho,Del Bosque mwenye umri wa miaka 62 amesema huenda akaendelea kucheza na mfumo wake huo huo. "Tutacheza na mshambuliaji," hiyo ni lazima na io wazi hata kama tutamtumia Na 9 feki au namba 9 wa ukweli,kama kanuni zilivyo lazima kila timu iwe na namba 9 ingawa kwetu sisi hatujampata tunaye mhitaji amesema. TENNIS-PARIS UFARANSA Rafael Nadal na Novak Djokovic wanakutana hii leo katika mechi ya nusu fainal ya michuano ya tennis ya french open inayosubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki kote duniani baada ya wote kushinda mechi zao za robo fainal. Bingwa mara saba Nadal alimtoa Stanislas Wawrinka kwa seti 6-2 6-3 na 6-1 wakati Mpnzani wake mcheza tennis namba moja dunian kwa sasa Novak Djokovic alimbwaga Tommy Haas kwa seti 6-3 7-6 na 7-5. Wawili hao wote wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa,kutokana na wote kukutana katika fainal mwaka jana na leo wanakutana tena katika nusu fainal,Wakati huo nusu fainal nyingine ya leo ni ile itakayo wakutanisha Jo-wilfred Tsonga na David Ferrer.
Posted on: Fri, 07 Jun 2013 15:07:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015