Baraza kuu la chama cha walimu nchini KNUT limeafikia kwa kauli - TopicsExpress



          

Baraza kuu la chama cha walimu nchini KNUT limeafikia kwa kauli moja kuwa mgomo wa walimu utaingia juma lake la nne kuanzia jumatatu hii baada ya jaribio lao kuafikiwa mwafaka na serikali kukosa kuzaa matunda.hata hivyo baraza hilo limesema litaendelea mbele na juhudi za kutanzua mgomo huo kwa kufanya mazungumzo na serikali. Ni uamuzi uliotarajiwa kusitisha mgomo wa walimu.Lakini mambo ni kinyume kwani wanafunzi wanaanza juma lingine la nne pasi na kujua ni lini walimu watarejea darasani . Hii ni baada ya walimu kususia ofa ya serikali kuwapa shilingi bilioni kumi na saba ili kuwashawishi kusitisha mgomo wao.Wanasema watarejea rasani iwapo serikali itatekeleza matakwa yao ya kuwalipa marupurupu wanayohitaji sambamba na mwafaka wa mwaka alfu moja mia tisa na tisini na saba. Na huku katibu mkuu wa chama cha knut mdzo nzili akikanusha madai ya mgomo huo kuingiliwa kisiasa,walimu hao wamesema mgomo huo utasitishwa iwapo baraza kuu litaafikia uamuzi kama huo na baada ya kukamilisha mazungumzo na serikali. Msimamo huu mkali unakisiwa kusababishwa na matamshi ya rais Uhuru Kenyatta aliyewaka wazi kuwa serikali haina fedha za kugharamia mahitaji ya walimu ambayo ni shilingi bilioni arobaini na tatu.
Posted on: Sun, 14 Jul 2013 13:28:31 +0000

Trending Topics




© 2015