Baraza la makanisa nchini NCCK linaunga mkono kuhairishwa kwa kesi - TopicsExpress



          

Baraza la makanisa nchini NCCK linaunga mkono kuhairishwa kwa kesi dhidi ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.Kupitia kwa katibu wake mkuu Peter Karanja,baraza hilo linasema kesi hizo zinafaa kuhairishwa angalau kwa mwaka mmoja ili kuwaruhusu wawili hao kutekeleza majukumu yao kikatiba.Kwa kuhairisha kesi hizo,NCCK linataka marekebisho kufanyiwa mkataba wa Roma uliobuni mahakama ya ICC.Kwa sasa waziri wa mambo ya nje Amina Mohamed yuko mjini New York, Marekani kutafuta uungwaji mkono kuhusiana na azma ya kuhairishwa kwa kesi hizo pendekezo linaloungwa mkono na mataifa ya afrika.
Posted on: Wed, 30 Oct 2013 15:17:43 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015