Beki wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya Yanga, - TopicsExpress



          

Beki wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya Yanga, Kevin Patrick Yondan amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 na kuzawadiwa donge nono la Sh. Milioni 5. Yondani ambaye alihamia Yanga akitokea Simba amechaguliwa kuwa mwanasoka bora VPL baada ya kuwa na msimu mzuri na klabu yake ya Yanga ambayo ilitwaa ubingwa huo huku akiruhusu mabao machache kuliko timu nyinginezo. Vodacom pia ilitoa tuzo kwa kocha na bora na wachezaji wengine waliofanya vizuri msimu uliopita na tuzo zilikuwa kama zifuatazo Top Scorer- Kipre Tchetche Azam (5m) Best Player- Kevin Yondani (5m) Best Coach Abdallah Kibadeni Kagera (7.5m), Best Goalkeeper- David Burhani Prisons (5m) Mchezaji mwenye nidhamu- Fulli Maganga JKT Ruvu (5m) Team yenye nidhamu- Yanga (15m)
Posted on: Thu, 04 Jul 2013 19:47:25 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015