Ben Wa Saanane anatukumbusha kuwa Uchaguzi Mkuu 2015 ni kati ya - TopicsExpress



          

Ben Wa Saanane anatukumbusha kuwa Uchaguzi Mkuu 2015 ni kati ya Lootocracy Vs Patriocracy. Kwa wanasiasa bila kujali itikadi ya chama chako jichunge usiwe upande mbaya wa historia Kundi la Lootocracy(Nimetohoa kutoka Neno Looting) lenye maana ya Wizi,Ufisadi,Ukwapuaji wa mali za Umma.Kundi Hili linaratibiwa na Watu wenye Historia ya Wizi wa Mali za Umma,Wenye Fedha zisizoelezeka walikozitoa maana hata Mwl.Nyerere alipowauliza mwaka 1995 hawakupata ujasiri wa kuelezea walikozipata,Wakwepa kodi,Watu Wanaojigamba na kukiri kuwa wao na watoto wao ni wauza Unga (Drugg Loards).Siku hizi limeongezewa nguvu na Wabakaji na Wauaji,Wazinzi na Waandishi wa habari makanjanja,Wamiliki wa Blog uchwara,Wanasiasa vijana wafuata mkumbo na waoga wa maisha,Waganga wa Kienyeji na Maprofesa wajinga pamoja na wasomi walioweka digrii zao mifukoni mwa mafisadi hawa na kuchimbia Weledi wao Ardhini,Kundi la wenye sifa za uvivu wa kufikiri na wasiokua na dira kwa nchi zaidi ya utapeli wa kisiasa na kulia machozi ya mamba kuhusu tatizo la ajira kwa vijana bila kujua kwa ufiasadi wao wamechangia kuongeza tatizo,waasisi wakubwa wa Shule za kata na wahunzi wa Div.5 mitaani .Ujasiri ulioje? Kundi hili linajivunia kuwa na watu wenye kufanya maamuzi magumu ya Kuliibia Taifa,Kusababisha Mgao wa Umeme,Wenye ujasiri wa kuiba na kurudisha Chenji makanisani na Misikitini kwa Manabii wala Rushwa(Kama wale manabii wa Baali Waliotabiriwa kwenye Biblia ). Kundi hili Linaona misingi ya Uongozi Shupavu kujenga taifa Kubwa la sasa na Baadae kupitia kigezo cha Flexibility,Responsibility and accountability kama ishara ya kifo kwao Imejaa Matapeli wa Kisiasa na Ma-Opportunist wa Kutisha wakiongozwa na wale waliopingwa na Baba wa Taifa Mwl.Nyerere.Walifurahi na Kuibuka baada ya Kifo chake wakapewa Mamlaka makubwa wakaonyesha true colours wakabanwa wakarudi nyuma wakilia machozi ya Mamba lakini pia wakahakisha umma ulioleta shinikizo nao unakiona cha moto kupitia Mgao wa Umeme.Kiongozi wao wanyetaka awe Rais anaweza kujikuta akiwa Nyapara wao Gerezani baada ya 2015 kama Patriocracy watajipanga vyema ba kuungana bila kujali itikadi za vyama vyao.Lootocracy hawataki hili litokee .Wapo tayari kuua.They are desperate than ever before. Leo wanataka Urais,Mmoja wao awe Commander-in-Chief.Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama yawe Chini yake,Mamlaka yake yasihojiwe Popote.What a joke! Patriocracy(Nimetohoa kutoka neno Patriot) kwa Upande Mwingine Linajumuisha Wazalendo,Wasomi wenye upeo na weledi katika misimamo,Waandishi nguli wanaoheshimu taaluma zao,Wanablog Maahiri wenye Misimamo wasiopenda kujipendekeza,Vijana shupavu na wenye jeuri linapokuja suala la nchi yao kama alivyowahi kusema Mwl.Nyerere ,Pia Wachangiaji makini kwenye mitandao kama Facebook na Twitter,Mihadhara na midahalo ya wazi,Maaskofu na Masheikh jasiri katika kuisimamia maandiko matakatifu,Pia walalahoi na Matajiri wazalendo Nilipofikia hapa nimemkumbuka Mwanamapinduzi Nguli na Kiongozi Shupavu aliyekaribia kuipiga Ulaya nzima na Mtaalamu wa Medani za Mapambano Napoleon Bonaparte.Umaahiri wake wa Mikakati ya Kisiasa na Vuguvugu la Mapambano kisiasa na Kivita alisema Let us wait a little,When your enemy is executing a false Movement,Never interrupt him(Hebu tusubiri Kidogo,Adui yako anapotekeleza harakati/vuguvugu la Uongo/kimakosa,Usimgutushe/usimshtue). Falsafa ya Napoleon Bonaparte ikitumiwa vizuri kuanzia Sasa hadi 2015...Baada ya Hapo Taifa Litapona na Kupata ukombozi wa Pili. Never Interrupt them. Kapteni wa Meli ya Kifahari ya Titanic alirudia Maneno ya wamiliki wa Meli na Wahandisi na kujigamba eti This Ship is Unsinkable.Lootocrats nao wamejigamba Meli yao Haizami eti wao ndio wamiliki (Rejea Watoto wetu wanauza unga nani wa kuwakamata,sisi ndio wenye nchi yetu).
Posted on: Thu, 21 Nov 2013 04:36:18 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015