Burundi imeweka wazi Msimamo wa kutoyatambua Maamuzi yoyote - TopicsExpress



          

Burundi imeweka wazi Msimamo wa kutoyatambua Maamuzi yoyote yatakayofanywa na Nchi za Kenya,Uganda na Rwanda kwa Mgongo wa Jumuia ya Afrika Mashariki kama hayatashirikisha Nchi ya Tanzania. Hayo yamewekwa wazi na Msemaji wa Serikali ya Burundi Bw. Philip Nzomaribwa. Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi Bi. Leote Nzoyimana amethibitisha hayo kwa Waandishi wa Habari wa Burundi na kusisitiza kwamba ana matumaini kwamba Tofauti za Jumuia hiyo zitapatiwa Ufumbuzi katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama utakaofanyika Novemba mwaka huu. SOURCE: DW. Hii ni move nzuri sana kwa viongozi wetu kama wana busara. Kwa kuwa tayari DRC wameonesha nia ya kuingia EAC lakini mpaka Tanzania iwepo na kwa kuwa BURUNDI wanakuwa nyuma ya mgongo wa Tanzania, hapa ndipo pa kucheza karata yetu. Kwamba wao wamemwaga ugali sisi tumwage mboga, tusitoke EAC lakini tuanzishe TANZANIAN BUSSINESS PARTNERS ambapo tutawachukua CONGO na BURUNDI kwa kuwa wote ni locked countries na matatizo yao yanafanana(vita vya ndani).Halafu tuingie mikataba na CONGO ya kiuchumi kabla ya kuipigia debe iingie EAC. Sisi tunachotakiwa kufanya CONGO ikishaingia kule ni kujenga kituo cha kibiashara kikubwa sana pale KAHAMA na hii inakua strategically kwa ajili ya ku-connect biashara ya Burundi na CONGO kupitia bandari ya Tanga huku tukianza ku-destabilize biashara ya Rwanda na Uganda kupitia Mombasa. Kama CONGO na Burundi zikiwa na amani na zikfanya biashara kupitia KAHAMA obvious kukua kwao kiuchumi kutaanza kuizorotesha RWANDA na UGANDA ambazo itabidi zinunue baadhi ya bidhaaa toka CONGO na BURUNDI ambazo zimepita Tanzania(KAHAMA). Na kwa vyovyote kwa mfumo wa free market hawawezi kundelea kupitisha bidhaa zao KENYA kwa kuwa ni gharama na chumi za nchi zinazowazunguka zimeshakua hivyo hawana jinsi isipokua kurudi KAHAMA. Wakija huku tunawa-force waingie mikataba ya kibiashara na TANZANIA BUSSINES PARTNERS wasipotaka waondoke, Lazima wataingia ili kunusuru chumi zao na hapa Tanzania itakua imewini game ya kutengwa na kuwa na sauti kubwa ya kiuchumi katika ukanda huu.
Posted on: Tue, 01 Oct 2013 11:32:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015