CAPITAL ONE CUP: CHELSEA YASHINDA, CITY YABAMIZA 7-0 ! - TopicsExpress



          

CAPITAL ONE CUP: CHELSEA YASHINDA, CITY YABAMIZA 7-0 ! CHELSEA 2 BOLTON WANDERERS 1 Chelsea wamesonga kwenye Capital One Cup baada ya kuichapa Bolton Wanderers Bao 2-1 Uwanjani Stamford Bridge. Chelsea walipata Bao Dakika ya 25 baada ya Kona kuleta kizaazaa na Sentahafu Kurt Zouma, akicheza Mechi yake ya kwanza, kukwamisha Mpira wavuni. Kwenye Dakika ya 31 Matt Mills aliisawazishia Bolton kwa Kichwa kufuatia Krosi safi. Oscar aliipa Chelsea Bao la 2 kwa Shuti la chichini katika Dakika ya 55. VIKOSI: Chelsea: Cech,Azpilicueta, Zouma, Cahill, Filipe Luis; Mikel, Ake; Salah, Oscar, Schurrle; Remy Akiba: Ivanovic, Hazard, Drogba, Matic, Schwarzer, Christensen, Baker Bolton: Lonergan, Mills, Moxey, Dervite, Herd, Danns, Pratley, Kamara, Feeney, Davies, Beckford Akiba: McNaughton, Ream, Spearing, Mason, Clayton, Kenny, Lee Chung-yong Refa: Graham Scott +++++++++++++++++++++++ MAN CITY 7 SHEFFIELD WEDNESDAY 0 Man City wametinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Capital One Cup kwa kishindo baada kuichapa Sheffield Wednesday Bao 7-0 Uwanjani Etihad. Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0. Kipindi cha Pili, Mkongwe Frank Lampard aliipa City Bao baada kuunganisha Mpira wa James Milner katika Dakika ya 47. City waliongeza Bao nyingine katika Dakika ya 53 kupitia Edin Dzeko, Jesus Navas, Dakika 1 baadae, na Penati ya Dakika ya 60 ya Yaya Toure baada ya Frank Lampard kuchezewa Rafu na Kamil Zayatte ambae alipewa Kadi Nyekundu. Mabao zaidi ya City yalifungwa na Jose Pozo, Dakika ya 88, na Lampard Dakika ya 90. VIKOSI: Man City: Caballero, Sagna, Demichelis, Mangala, Kolarov, Navas, Fernandinho, Lampard, Milner, Toure, Dzeko Akiba: Hart, Kompany, Sinclair, Clichy, Boyata, Bytyqi, Pozo Sheffield Wednesday: Kirkland, Buxton, Zayatte, Lees, Mattock, Palmer, Coke, Maguire, Maghoma, Madine, May Akiba: Westwood, Semedo, Nuhiu, Drenthe, Helan, Hope, Dielna Refa: Paul Tierney CAPITAL ONE CUP – RAUNDI YA TATU MATOKEO: FT Burton Albion 0 - 3 Brighton & Hove Albion half-time: (0 - 2) match details : 18 0 - 1 Rohan Ince 37 0 - 2 Kazenga LuaLua 66 0 - 3 Craig Mackail-Smith 87 Inigo Zapateria Calderon FT Tottenham Hotspur 3 - 1 Nottingham Forest half-time: (0 - 0) match details : 62 0 - 1 Jorge Grant 72 Ryan Mason 1 - 1 83 Roberto Soldado 2 - 1 90 Harry Kane 3 - 1 AET Crystal Palace 2 - 3 Newcastle United half-time: (1 - 1) extra-time: (0 - 1) match details : 25 (pen.) Dwight Gayle 1 - 0 36 1 - 1 Emmanuel Riviere 48 1 - 2 (pen.) Emmanuel Riviere 90 KaiKai 2 - 2 100 Mehdi Abeid 112 2 - 3 Paul Dummett FT West Bromwich Albion 3 - 2 Hull City half-time: (1 - 1) match details : 15 Brown Ideye 1 - 0 41 1 - 1 Thomas Ince 50 1 - 2 Robert Brady 88 Gareth McAuley 2 - 2 89 Saido Berahino 3 - 2 MATOKEO: Jumanne Septemba 23 Arsenal 1 Southampton 2 Cardiff 0 Bournemouth 3 Derby 2 Reading 0 Leyton Orient 0 Sheffield United 1 Liverpool 1 Middlesbrough 1 [Baada ya Dakika 120, 2-2, Penati 14-13] MK Dons 2 Bradford 0 Shrewsbury 1 Norwich 0 Sunderland 1 Stoke 2 Swansea 3 Everton 0 Fulham 2 Doncaster 1 CAPITAL ONE CUP: DROO YA RAUNDI YA MTOANO TIMU 16 YAFANYIKA ! DROO ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya CAPITAL ONE CUP imefanyika Usiku wa jana na hakuna Vigogo waliokutanishwa labda ile Mechi ya Timu za Ligi Kuu England, Liverpool v Swansea City. Mechi za Raundi hii zitachezwa Wiki ya kuanzia Oktoba 27. ++++++++++++++++++++++++++ DROO YA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16: Man City v Crystal Palace au Newcastle Fulham v Derby Liverpool v Swansea MK Dons v Sheffield United Bournemouth v West Brom Shrewsbury v Chelsea Tottenham v Brighton Stoke v Southampton ++++++++++++++++++++++++++
Posted on: Thu, 25 Sep 2014 08:17:45 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015