CHANGAMOTO ZA MFUKO WA KUHIFADHI WANYAMA PORI - TopicsExpress



          

CHANGAMOTO ZA MFUKO WA KUHIFADHI WANYAMA PORI TANZANIA Sijaridhika na maelezo katika vifungu vifuatavyo; Katika kutekeleza majukumu yake, Mfuko unakabiliwa na changamoto mbalimbali. Changamoto kubwa ni mbili kama ifuatavyo: 7.1 Kutokana na mabadiliko ya hali ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuwepo kwa teknolojia ya mawasiliano ya simu za mkononi mahitaji ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na wimbi la ujangili nchini na makubwa ukilinganisha na miaka ya 80 na 90. Kutokana na hali hiyo Mfuko hauna uwezo wa kukidhi mahitaji ya fedha kwa ajili ya kuzuia ujangili hususan fedha za kununua vifaa vya doria (magari, radiocalls, mahema, sare), mafuta ya magari na ndege pamoja na malipo ya posho ya kujikimu ya wahifadhi wanyamapori. 7.2 Chanzo kikuu cha mapato cha Mfuko ni 25% ya mapato yatokanayo na biashara ya uwindaji wa kitalii. Biashara ya uwindaji wa kitalii hutegemea wateja ambao ni matajiri kutoka nchi za Ulaya na Marekani. Mtikisiko wowote wa kisiasa, kiamani au kiuchumi unapotokea katika nchi ambazo watalii hao wanatoka huathiri hali ya uwindaji nchini na hivyo mapato ya Mfuko huporomoka. Tunahitaji kufikiria zaidi kuleta mabadiliko na ufanisi katika mfuko huu
Posted on: Fri, 30 Aug 2013 19:09:58 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015