CHOMBEZO:CHINGA MTUNZI:JUNIOR NICKSON KING SEHEMU YA - TopicsExpress



          

CHOMBEZO:CHINGA MTUNZI:JUNIOR NICKSON KING SEHEMU YA TANO. ************************** Nakumbuka siku hiyo nilichelewa kutoka mtaani..Endela,,, Wakati niko njiani kurudi nyumbani huku nikiwa nimechoka sana mara nikasikia honi ya gari nyuma yangu. Nikasogea pembeni ili lipite, lakini badala ya kupita likasimama usawa wangu, nikataka kupiga hatua ili niendelee na safari yangu lakini nikaona kioo cha gari kikishuka na hapo ikaonekana sura ya mama Zaituni ambaye alikuwa ni mteja wangu sana mtaa wa tatu kutoka nilipokuwa nikiishi mimi. Basi nikasogea karibu na gari lake, tukapeana salamu ya uchangamfu sana kwani ilikuwa imepita kama wiki mbili sijapita mtaani kwake. Baada ya salamu akaniambia kuwa nipande kwenye gari ili nikawapakae rangi wadogo zake wawili waliotoka kijijini kwa ajili ya harusi ya rafiki yake. Kiukweli kwa jinsi nilivyokuwa nikijisikia hata zile fedha alizonihahidi sikuona umuhimu wake, nikamuomba kuwa kesho yake asubuhi na mapema nitadamkia nyumbani kwake ili kufanya kama alivyoomba. Hakuhoji zaidi badala yake akachomoa noti ya elfu kumi na kunikabidhi huku akinihahidi kesho yake atakuja kunichukua kwa gari. Tukaagana na kila mmoja akaendelea na safari yake. Kiukweli usiku wa siku hiyo sikulala kabisa, mawazo yangu yote yalikuwa kwa mpenzi wangu Noela. Nilipoona mawazo yamezidi nikanyanyuka kitandani na kwenda hadi lilipokuwa begi langu la nguo kisha nikatoa picha zake na kurudi nazo pale kitandani. Nikaona njia sahihi ya kujiliwaza ni kuziweka kifuani kwangu lakini bado haikunisaidia, nikajaribu kumpigia simu angalau niisikie tu sauti yake lakini iliita bila kupokelewa hadi nikakata tamaa kwani nilijaribu zaidi ya mara saba bila majibu. Nikamwandikia meseji ili angalau kama atakuwa yupo mbali na simu yake basi akirudi ujumbe umfikie kimaandishi, "Noela, ni miezi mitatu tangu upotee machoni mwangu, kula imekuwa tabu kwangu,kazi nafanya kwa shida naukumbuka sana uwepo wako machoni mwangu, kiukweli hiyo miaka mitatu utakayoishi huko naiona kama miaka hamsini, kumbuka pasipo wewe mimi si kitu, tafadhali uonapo meseji hii usisite kunijibu kwa kuniambia, mimi ni wako tu Junior" sms hii nilimuandikia kwa uchungu sana kwani tangu alipoondoka mawasiliano yangu na yeye hayakuwa mazuri kama mwanzo. Nilipomaliza kumtumia meseji ile, sikujua kilichoendelea tena mpaka pale niliposikia alarm ya simu yangu ambayo huwa inaniamsha kila itimiapo saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Nikapiga magoti pale kitandani na kumshukuru mungu kwa kuniamsha salama kisha nikajiinua pale kitandani na kuchukua kindoo changu cha bafuni na kwenda kujimwagia maji. Nilipotoka bafuni na kuvaa nguo zangu tayari kwa kuingia mtaani asubuhi na mapema ile, nikachukua vitu vyangu na kutoka nje nikiwa na mawazo tele juu ya Noela ambaye hakujibu sms yangu niliyomtumia usiku. Hata sikutembea hatua kumi nikaona gari la mama Zaituni likija kwa mwendo wa taratibu, nikaona angalau atakuwa amenipunguzi kutembea mwendo mrefu hadi kwake. Alipofika karibu akasimama na kunifungulia mlango kisha nikazama ndani, akageuza gari na safari ikaanza. Nilipoingia mle ndani tukapeana salamu huku gari ikiwa inazidi kuisulubu ardhi, baada ya mama Zaituni kuona niko kimya huku nikiwa mwenye mawazo sana akaweka wimbo wa, "nimekuchagua wewe" uliyoimbwa na Bob Ludara. Wimbo ule uliniamsha hisia kali na kujikuta nikiuimba kwa kuweka jina la Noela ndani yake huku machozi yakinitiririka mashavuni mwangu, lakini wakati nakazana kuimba na machozi yakizidi kumwagika nikahisi mkono laini ukipangusa machozi juu ya mashavu yangu na machoni. Nikaacha kuimba na kuangalia ni kitu gani kinaendelea kwani nilikuwa nimehamishia mawazo yangu mbali sana. Nikashuhudia mama Zaituni akiwa amepaki gari bembeni mwa njia huku akiwa amenisogelea kabisa na viganja vyake vikizidi kutalii mashavuni mwangu huku akiniuliza ni nani yangu huyo ninayemuimba? Sikusita kumweleza kila kitu na hii ni kutokana na kwamba mama Zaituni alikuwa na umri mkubwa sawa na wa mama yangu mzazi. Stori ile niliyompa ilimhuzunisha sana lakini mwisho akaniambia, "usijali". Sikuendelea kutoa machozi baada ya kauli ile ya mama Zaituni, nikamuomba awashe gari tuendelee na safari ili niwahi kumfanyia kazi yake kabla ya kuwazungukia wateja wengine. Kama nilivyomuomba ndivyo alivyotekeleza, akawasha gari na safari ikaendelea. Tulipofika nyumbani kwake na kuingia ndani nilishindwa kujizuia kushangaa kwani nyumba ilikuwa kimya kabisa, namaanisha hapakuwa na mtu yeyote na hii ilijidhihirisha tulipozama ndani kabisa na yeye kunikaribisha kwenye sofa kubwa lililokuwa mle sebuleni. Mimi: Mbona siwaoni hao ulioniambia nije kuwapakaa rangi? Mama Zaituni: Mbona una haraka? Huku akiingia chumbani, "subiri nikawalete" sikusubiri sana kwani baada ya dakika kadhaa akarudi akiwa ndani ya khanga moja mwilini mwake, hali iliyonifanya nisisimkwe na mwili kupita maelezo. Kiukweli yule mama alikuwa ameumbika haswa, sasa alipoingia ndani ya khanga ndo ikazidi kuwa balaa. Haya sasa mambo ndo hayo. Itaendelea like&coment
Posted on: Mon, 09 Sep 2013 15:22:18 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015