COCOJAMBO ASUBUHI HII: ALHAMIS, 12.09.2013: (HABARI). Mitihani ya - TopicsExpress



          

COCOJAMBO ASUBUHI HII: ALHAMIS, 12.09.2013: (HABARI). Mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa wanafunzi wa darasa la saba imeanza rasmi kufanyika nchi nzima huku baadhi ya viongozi wa wizara ya elimu na mafunzo wakifanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya shule. Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej leo amezindua Bodi mpya ya Makamishna wa Tume ya Ukimwi Zanzibar na kuitaka kushirikiana kwa karibu zaidi na wadau mbali mbali kuanzia ngazi ya chini ili kuhakikisha maambukizi ya janga la Ukimwi yanapungua na kufikia lengo la Zanzibar bila Ukimwi inawezekana. Jeshi la Polisi la Uturuki limetoa ufadhili wa masomo kwa askari kumi na saba ( 17) wa Jeshi la Polisi Tanzania kupata mafunzo mbalimbali yakiwemo ya upelelezi wa wahalifu na mbinu za uchunguzi wa kimaabara pamoja na usimamizi na uendeshaji wa gari la matukio yatakayochukua muda wa mwezi mmoja nchini Uturuki. Waasi wa kundi la Al-Nusra lenye mafungamano na Al-Qaeda wamewauwa watu 12 kutoka madhehebu ya Alawi ambayo ni sehemu ya madhehebu ya Shia nchini Syria. Bomu lililotegwa garini limeripuka jana nje ya jengo moja lililowahi kuwa ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi, Libya, katika kile maafisa walichosema ni onyo kwamba maafisa wa kibalozi hawako salama. Mtangazaji wa Redio nchini Kenya, Joshua Arap Sang, anayeshtakiwa kwa maovu dhidi ya binaadamu pamoja na Makamu wa rais wa nchi hiyo, William Ruto, alishikilia kwamba upande wa mwendesha mashitaka hauna hoja dhidi yake. MAONI: +255 772389889.
Posted on: Thu, 12 Sep 2013 03:44:12 +0000

Trending Topics



-Windows-7-Beginners---wikiHow-5-days-ago-topic-1517153068548375">How to Install Windows 7 (Beginners) - wikiHow 5 days ago ...
(5) Jacqueline Walker ow.ly/t3q0g This is my skinny fiber
monstermmorpg/Screenshots Avia (Japanese: ツバサの国
"Eu vou torcer Aqui eu ergui meu templo para vencer Eu já lutei
I was so intrigued by the UAAP 77 peps squad competition yesterday

Recently Viewed Topics




© 2015