COCOJAMBO ASUBUHI HII: ALHAMIS, 22.08.2013: (HABARI). Wananchi wa - TopicsExpress



          

COCOJAMBO ASUBUHI HII: ALHAMIS, 22.08.2013: (HABARI). Wananchi wa Shehia ya Kombeni Wilaya ya Magharibi wameilalamikia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kutokana na tatizo la maji linaloendelea kuwakabili kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa na kusababisha kuzorotesha harakati zao za kiuchumi. Baraza Kuu la Uongozi la CUF linakutana jijini Dar es Salaam kwa kikao chake cha kawaida cha siku mbili. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kuona changamoto zinazowakabili watendaji wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliopo Dar es salaam zinashughulikiwa vyema kwa kupatiwa ufumbuzi ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Posted on: Thu, 22 Aug 2013 04:42:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015