COCOJAMBO ASUBUHI HII: JUMATATU, 19.08.2013: KIMATAIFA: Katibu - TopicsExpress



          

COCOJAMBO ASUBUHI HII: JUMATATU, 19.08.2013: KIMATAIFA: Katibu mkuu wa wizara ya Afrika mashariki Dk. Stergomena Tax ameapishwa rasmi kuwa katibu mtendaji wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC ambapo atakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo. Muungano wa makundi ya itikadi kali umefutilia mbali maandamano yaliyoitishwa kote nchini Misri, kulalamika dhidi ya jeshi. Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa waliopewa jukumu la kuangalia kama silaha za kemikali zimetumiwa katika mzozo wa Syria,wamewasili Damascus jana. Robert Gabriel Mugabe ataapishwa rasmi Alkhamisi ijayo kwa muhula mwengine wa miaka mitano kama rais wa Zimbabwe. MAONI: +255 772389889.
Posted on: Mon, 19 Aug 2013 04:20:25 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015