COCOSPORTS USIKU HUU: ALHAMIS, 21.11.2013: (Saa 2 kamili usiku - TopicsExpress



          

COCOSPORTS USIKU HUU: ALHAMIS, 21.11.2013: (Saa 2 kamili usiku huu). Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu. Mechi ya kirafiki ya kimataifa ya FIFA Date kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (The Warriors) iliyochezwa juzi (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 50,980,000 kutokana na watazamaji 7,952. JUMAMOSI Usiku, ndani ya Signal Iduna Park, Wenyeji Borussia Dortmund watawakaribisha Mabingwa wa Germany, Bayern Munich, katika Mechi ya Ligi ya Bundesliga. MCHEZAJI BORA DUNIANI, Lionel Messi, ametoa sifa kubwa kwa Cristiano Ronaldo kwa ufungaji wake Mabao kila kukicha. ALFAJIRI ya leo, Uruguay ilitoka Sare ya 0-0 na Jordan, hivyo kufuzwa kwa Jumla ya Bao 5-0, na kukamilisha Nchi 32 zitakazocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil kuanzia Juni 12 ambapo Ratiba ya michuano hii ipo tayari Siku nyingi na Desemba 6 itafanyika Droo maalum kupanga Makundi manne ya Timu 4 kila moja. Brazil, kama Wenyeji, wao tayari wapo Kundi A.
Posted on: Thu, 21 Nov 2013 16:48:04 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015