COCOSPORTS USIKU HUU: JUMAPILI, 14.07.2013: (Saa 3 kamili - TopicsExpress



          

COCOSPORTS USIKU HUU: JUMAPILI, 14.07.2013: (Saa 3 kamili usiku). Mechi ya kwanza mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) iliyochezwa jana (Julai 13 mwaka huu) imeingiza sh. 113,268,000 kutokana na watazamaji 17,121. Timu ya Taifa (Taifa Stars) imeondoka leo asubuhi (Julai 14 mwaka huu) kwenda Mwanza ambapo itapiga kambi ya siku kumi kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Uganda (The Cranes) kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini. KATIKA Mechi yake ya kwanza na Klabu yake mpya, Meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini, ameambua kipigo cha Bao 2-0 kutoka kwa SuperSport ya Afrika Kusini hii leo ndani ya Loftus Versfeld Stadium huko Pretoria. MASHINDANO Ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Vijana chini ya Miaka 20, U-20, Jana Usiku yalimalizika Nchini Turkey kwa Fainali iliyoisha 0-0 katika Dakika 120 ndani ya Türk Telekom Arena Ali Sami Yen Spor Kompleksi Mjini Istanbul na France kuibuka kidedea kwa kuitoa Uruguay kwa Mikwaju ya Penati 4-1. David Moyes, Meneja mpya wa Manchester United ambae Jana alianza Mechi yake kwa kuchapwa 1-0 na Singha All Stars XI huko Bangkok, Thailand, amesema hakuhuzunika na kipigo hicho lakini amevutiwa a baadhi ya Wachezaji huku akimsifia sana Chipukizi Wilfried Zaha.
Posted on: Sun, 14 Jul 2013 16:36:59 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015