COCOSPORTS USIKU HUU: JUMATANO, 14.08.2013: Kamati ya Uchaguzi ya - TopicsExpress



          

COCOSPORTS USIKU HUU: JUMATANO, 14.08.2013: Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokuwa ikutane jana (Agosti 13 mwaka huu) na leo (Agosti 14 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza sasa itakutana keshokutwa (Agosti 16 mwaka huu) saa 4 asubuhi. MSHAMBULIAJI machachari wa Liverpool, Luis Suarez, inadaiwa leo amegeuka kabisa na kudaiLUIS_SUAREZ-KILIO atabakia Liverpool na wakati huo huo leo kuifungia Nchi yake Uruguay Bao moja ilipocheza na Japan huko Miyagi Stadium, Rifu, Japan. Kocha wa Brazil,Felipe Scolari ametabiri kuwa nyota wa Barcelona,Lionel Messi ataendelea kuwa mchezaji bora wa dunia kwa miaka miwili tena ijayo. KLABU ya Ukraine Metalist Kharkiv imetimuliwa kutoka michuano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kufuatia uchunguzi wa upangaji matokeo Mechi. KIUNGO Michael Carrick amejitoa kwenye Kikosi cha England ambacho leo Usiku kinacheza na Mahasimu wao wakubwa Scotland ambao hawajakutana nao tangu Novemba 1999. Klabu ya Napoli pia inaonyesha nia ya kuipiku Arsenal katika kumsajili Kiungo Mkabaji, Gustavo ambae ofa yake ilikubaliwa na Bayern ilia Arsenal waongee nae.
Posted on: Wed, 14 Aug 2013 16:43:01 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015