Chozi la Tunu ... 6 .... Tunu alirudi akiwa na wasiwasi mkubwa - TopicsExpress



          

Chozi la Tunu ... 6 .... Tunu alirudi akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya uso wake. Mtu wa kwanza kukutana naye, alikuwa ni Veridiana aliyekuwa eneo la jikoni ambapo alikuwa anaandaa chakula cha usiku. Tunu aliufungua mlango wa nyavu kwa kuwa ule wa mbao ulikuwa wazi, akakutana uso kwa uso na Veridiana yeye akiwa katika mwendo wa kunyata. Tunu! Veridiana alimshitua kwa kuwa Tunu alikuwa hajafahamu kuwa jikoni hapo yupo mtu anayemuona alivyokuwa akinyata. Enhe!! Tunu akashituka macho yakamtoka pima hata viatu alivyovivua na kuvishika mkononi, vikamponyoka. Vipi mbona unanyata? Anha ah! Tunu alikuwa akikataa hamna kitu Tunu akazuga zuga pale bila sababu ya msingi na Veridiana aliliona hilo. Veridiana alijawa wasiwasi sana na kujiuliza kwanini Tunu anaonekana mwenye wasiwasi kiasi hicho? Akamuuliza Yuko wapi Kishubi? Tunu alisimama alipokuwa ameanza kupiga hatua za kuondoka na kugeuka nyuma kana kwamba sauti ya swali aliloulizwa ilitokea nyuma ya mgongo wake. Enhe! Kishubi? Akauliza kijinga hajarudi? Mimi nimepata masahibu makubwa sana naomba tu uniache kwa kweli nimeachana na kishubi mapema sana Akamuacha Veridiana akiwa anamshangaa na kuingia zake chumbani. Yeye Tunu, tangu siku ile alidhani kuwa yale yaliishia pale pale jikoni, lakini kumbukumbu hiyo haikutoka kichwani mwa Veridiana mpaka leo ambapo amekumbwa na tukio la kufuatiliwa na muuaji wa Ndibuweza. Akiwa katika giza zito akauinua mkono wake wa kushoto, ulibaki kibubutu pekee. Mkono huo ulikatwa katika harakati za kutafuta ukweli wa wapi alipo Kishubi. Chozi likamtoka na kumlaani Tunu kwa kuwa na roho mbaya kiasi kile. Kuukata mkono wake kwa imani za kishirikina. Kama pesa alikuwa nayo, kwanini aukate mkono wake? Kwa shida ipi? Mwanzo hayo yote hakuwa na majibu nayo lakini akabaki na labda .. Labda.. Kichwani mwake.
Posted on: Tue, 19 Nov 2013 06:14:40 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015