DAR ES SALAAM Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini - TopicsExpress



          

DAR ES SALAAM Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania. Pia ni jina la Mkoa wa Dar es Salaam. Ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania wakati Dodoma ni makao makuu ya Tanzania tangu mwaka 1973. Mpango wa kuhamisha serikali kwenda makao makuu mjini Dodoma bado unaendelea japokuwa bado ofisi nyingi za serikali ikiwa ni pamoja na Ikulu zipo Dar es Saalaam. Historia Makala kuu ya: Historia na Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam Jiji hili zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu دار السلام (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari). Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo pana ya mto Kurasini. Kuanzia 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu 1904 ziliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara kuwa koloni ya Tanganyika chini ya Uingereza. Wakazi na uchumi Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni tatu. Ingawa Dodoma inafahamika kama ndio mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam ndiko ziliko ofisi kuu za viongozi wa serikali, mabalozi, mashirika ya kimataifa, n.k. Uwanja wa ndege mkuu wa Tanzania uko pia mjini hii ni Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. Bandari ya Dar es Salaam katika bahari ya Hindi, ndio bandari kubwa nchini Tanzania inayojihusisha na usafirishaji na uingizaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, ujenzi, magari, madawa, n.k. Kiutawala, Dar es Salaam imegawanywa katika wilaya za Temeke, Ilala, na Kinondoni
Posted on: Mon, 22 Jul 2013 18:24:21 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015