DONDOO 09092013 1.ALIYEKUA MKUFUNZI WA HARAMBEE STARS NA PIA - TopicsExpress



          

DONDOO 09092013 1.ALIYEKUA MKUFUNZI WA HARAMBEE STARS NA PIA MKURUGENZI WA KIUFUNDI WA SPARKI YOUTH MOHAMED KHERI AMESEMA YUKO TAYARI KUFANYA KAZI NA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI KUIMARISHA HALI YA SOKA KOTE NCHINI KHERI AMBAE MARUFUKU YAKE ILIONDOLEWA NA FKF AMESEMA KWAMBA HANA BIFU NA SHIRIKISHO HILO NA YUKO TAYARI KWA NAFASI YOYOTE ILI KUENUA VIWANGO VYA SOKA HAPA MKOANI NA TAIFA ZIMA KWA JUMLA KHERI AMEMLIMBIKIZIA LAWAMA CHUNGU NZIMA ALIEKUA MWAKILISHI WA PWANI KATIKA KAMATI KUU YA FKF HUSSEIN TERRY KWA MASAIBU YAKE 2.MWAKILISHI WA SOKA YA KINA DADA MKOANI PWANI ASHA PILI AMETAKA KUTENGWA KWA ASILIMIA 2 YA FEDHA ZA CDF ANGALAU KUFADHILI MIRADI YA MAENDELEO YA SOKA KWA KINA DADA HAPA MKOANI ILI KUJIENDELEZA KITALANTA BADALA YA KUSHIRIKI KATIKA MAOVU ASHA PIA AMEBAINISHA KWAMBA TAYARI WANATAYARISHA MAPENDEKEZO YA KUIMARISHA SOKA YA WANAWAKE HAPA MKOANI VILE VILE MWAKILISHI HUYO AMEMUOMBA GAVANA WA KAUNTI YA MOMBASA ALI HASSAN JOHO KUKAA NA WABUNGE WAKE ILI KUOKOA KINA DADA KIMICHEZO HAPA MOMBASA INSERT….SUPPORT PILI KWA UPANDE WAKE MWAKILSHI WA FKF WA WANAWAKE KAUNTI YA MOMBASA LILIAN NANDUNDU AMESEMA KUHARIBIKA KWA MICHEZO KATIKA NGAZI ZA KITAIFA NI KWAMBA MASHINANI KUMEPUUZWA LILIAN AMEDAI KWAMBA KUNA TALANTA NYINGI ZA SOKA KWA AKINA DADA HAPA MKOANI LAKINI UKOSEFU WA UFADHILI NDIO KIKWAZO KIKUBWA KUIMARISHA SOKA HIYO AKIPIGIA MFANO MWANASOKA CHIPUKIZI WA MOMBASA OLIMPIC MWANAHALIMA ADAMS AMBAE KWA SASA NI MINGONI MWA WASICHANA WAWILI TU WA KENYA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CAMP YA MANCHESTER UNITED INSERT..NANDUNDU 3.SOGORA WA UFARANSA ZINEDINE ZIDANE AMESEMA KWAMBA LICHA YA KIUNGO FRANK LAMPARD KUTINGA UMRI WA MIAKA 35 NDIE MCHEZAJI MKUU KATIKA TIMU YA TAIFA YA UINGREZA KIUNGO HUYO WA CHELSEA ANATARAJIWA KUSHUKA UWANJANI KATIKA MECHI YAKE YA 100 KWA UINGREZA KUFUZU KWA DIMBA LA DUNIA HAPO KESHO JUMANNE DHIDI YA UKRAINE MJINI KIEV ZIDANE AKIZUNGUMZA KATIKA KIPINDI CHA BBC PIA AMEMTAJA LAMPARD KAMA KIONGOZI VILE VILE AMEBASHIRI UINGREZA WATAFUZU KWENYE DIMBA LA DUNIA NCHINI BRAZIL LAKINI HAITAKUA RAHISI HIVYO HUKO BRAZIL WAKATI HUO HUO ZIDANE AMESEMA ANAONELEA AIDHA CRISTIANO RONALDO AU FRANK RIBBERY KUSHINDA TUZO LA BALON DOR MWAKA HUU TIMU BORA KUTOKA KILA KUNDI ITAFUZU HUKU NAMBARI MBILI AKICHEZA PLAY OFFS 4.BINGWA WA UHISPANIA BARCELONA WANATARAJI KUTANGAZA MKATABA MPYA KWA KIUNGO ANDRES INIESTA MWANASOKA HUYO MWENYE UMRI 29 AMBAE TAALUMA YAKE YOTE NI CATALUNYA MKATABA WAKE NI BARCA UNAISHA MWAKA WA 2015 RAIS WA BARCELONA SANDRO ROSSEL AMEIMBIA RUNINGA MOJA NCHINI HUMO KWAMBA HIVI KARIBUNI WATAAFIKIA HILO 5.MSHAMBULZI WA CHELSEA NA CAMEROON SAMUEL ETOO HUENDA AKASTAAFU KUTOKA SOKA YA KIMATAIFA HAYA NI KULINGA NA TAARIFA NILIYOINUKUU KUTOKA JARIDA MOJA KWA JINA L’EQUIPE KWENGINEKO NI KWAMBA MENEJA WA MANCHESTER UNITED DAVID MOYES ANATAPANGA KUMSAJILI CHRISTIAN BENTEKE SIKU ZA USONI NA KUMKABIDHI JEZI NAMBARI 9 MGONGONI HUKU HALI YA BAADE YA WAYNE ROONEY IKISEMEKANA KUWA KATIKA ATI ATI TAARIFA HIZI NIMEZINUKUU KUTOKA KWA DAILY MIRROR WAKATI HUO HUO TAARIFA KUTOKA KWA DAILY TELEGRAPH ZINASEMA KWAMBA HUENDA MANCHESTER UNITED IKAMUONGEZEA KANDARASI WAYNE ROONEY AMBAE MKATABA WAKE UNAISHA MWAKA WA 2015 6.MCHEZAJI WA AS ROMA DANIEL DE ROSSI NI MCHEZAJI ANAELIPWA DONGE NONO NCHINI ITALIA KULINGANA NA TAKWIMU AMBAZO ZIMETOLEWA LEO KIUNGO HUYO MWENYE UMRI WA 30 KWA KIMA ANATINGA URO MILIONI 6.5 KWA MWAKA AKIMSHINDA MWENZAKE WA KARIBU URO MILIONI 1 MCHEZAJI WA NAPOLI GONZALO HIGUAN NA URO MILIONI 2 ZAIDI YA KAPTENI WAKE FRANCESSCO TOTTI HATA HIVYO NI KWAMBA LIGI KUU YA ITALIA HAINA MSHIKO WA FEDHA KULINGANA NA TAKWIMU HIZO ZILIZOTOLEWA HUKU WACHEZAJI 12 KATIKA TAIFA HILO WAKIPOKEA ZAIDI YA URO MILIONI 4 KWA MWAKA UKILINGANISHA NA WACHEZAJI 13 WA CHELSEA WANAOPATA KIASI SAWA NA HICHO SASA TUANGALIE ORODHA YA WACHEZAJI NA JINSI WANAVYOPOEKA MIPESA YAO KWA MWAKA KATIKA ITALY SERIA A 1. Daniele De Rossi Roma €6.5m 2. Gonzalo Higuain Napoli €5.5m 3. Diego Milito Inter €5m 4. Esteban Cambiasso Inter €4.5m 4. Carlos Tevez Juventus €4.5m 6. Francesco Totti Roma €4.5m 7. Mario Gomez Fiorentina €4.25m 8. Gianluigi Buffon Juventus €4m 8. Mario Balotelli Milan €4m 8. Kaka Milan €4m 8. Philippe Mexes Milan €4m 8. Marco Borriello Roma €4m 7.TUKISALIA NA TAARIFA IYO HIYO YA MISHAHARA YA WACHZAJI MSIKILIZAJI WANGU WA SPOTI NI KWAMBA HAKUNA MCHEZAJI KUTOKA LIGI KUU ITALIA AMBAE YUKO KATIKA ORODHA YA WACHEZAJI 10 BORA MASONKO BARAANI ULAYA KWA MFANO ZLATAN IBRAHIMOVIC WA PSG BAADA YA KUKATWA USHURU KWA MWAKA ANATIA MFUKONI URO MILIONI 14 SAWA NA MSHAMBULIZI WA MONACO RADAMEL FALCAO LIONEL MESSI KWA MWAKA ANATINGA URO MILIONI 13 HUKU GARETH BALE AKISHIKILIA NAFASI YA 9 BARANI ULAYA KWA DONGE NONO AKITIA MFUKONI URO MILINI 11 KWA MWAKA VILABU VYA JUVENTUS NA AC MILAN NDIVYO HUTUMIA KIMA KIKUBWA KULIPA MISHAHARA WACHEZAJI WAKE HUKU JUVE WAKITUMIA URO MILIONI 49.8 HUKU AC MILAN WAKITUMIA URO MILIONI 47.94
Posted on: Mon, 09 Sep 2013 17:25:46 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015