Daah leo nimepata zali kuna mdada mmoja kanifananisha nimefurahi - TopicsExpress



          

Daah leo nimepata zali kuna mdada mmoja kanifananisha nimefurahi balaa nimetoka zangu home nna pensi yangu ya turubai juu nna tisheti yangu ya HAKATWI MTU chini nimevaa yebo yebo zangu nyekundu juu kama kawaida nna kofia ya mkeka Nimepanda daladala nikakaa siti moja na mdada mmoja mzuri balaa nikawa namwangalia kwa jicho la uwizi nikaona na yeye ananiangalia huku ananichekea nikajua tayari kashanishobokea Kufika mbele kidogo nikaona ngoja nianze kumchokonoa nikamsalimia mrembo mambo akaitikia pouwa kaka yangu alafu samahani kama nakufananisha hivi ndo maana mda mwingi nakuangalia nikamuuliza unanifananisha na nani mrembo?? Akaniambia na mkaka mmoja hivi wa bongo movie filamu zake nyingi sana alikuwaga anapenda kuigiza na marehemu kanumba Nikacheka kidogo nikamwambia wala hujakosea dada ndo mimi yani hivi ninavyokwambia naelekea posta location kuna movie yangu naenda kumalizia Yule demu akaniambia hongera sana kaka unaigiza vizuri sana yani mm nakupendaga balaa nikionaga movie upo wewe lazima ninunue nikamwambia asante sana dada si unajua watu tumezaliwa na vipaji vyetu akaniambia kweli kaka hongera sana naomba namba yako basi alivyoniomba namba nikaogopa kutoa lisimu langu la kichina likubwa kama redio nikachukua simu yake nikasave namba yangu nimefurahi sana mrembo mzuri kama yule kunifananisha mimi na muigizaji wa bongo movie Tumefika mitaa ya tazara gari imesimama kituoni nimeshangaa namuona baba na mama wamepanda kwenye gari wapo na matenga ya nyanya nimestuka sana nikajua tayari mambo yameharibika Mama alivyoniona akaniuliza we chogo ndizi unaenda wapi asubuhi yote hii vyombo nyumbani umeosha umefagia kwenye mabanda ya kuku na yale matembele niliyokuambia uchambue uyapike tayari?? Nikabaki tu nimetoa macho abiria wote wananiangalia mimi yule demu akabaki tu ananishangaa baba kanifwata hadi pale kwenye siti niliyokaa kanipiga bonge la kofi akaniambia teremka haraka rudi nyumbani gongo la mboto sisi tumekuacha nyumbani tunajua unafanya kazi kumbe unaenda kuzurura mshua kanitoa pale kwenye siti huku kanikunja ananipiga makwenzi amenishushia pale pale tazara kituoni abiria wote wamebaki wanacheka Nimeanza kurudi home huku nalia njiani mama na baba wameniaibisha sana mrembo tayari alikuwa kashanishobokea nimeshampa na namba yangu wamekuja kuniharibia mwisho wa mchezo daah nimefika home nimejilalia chumbani kwangu sijui nitapata lini tena zali kama nililolikosa leo GONGA LIKE /SHARE/KAMA UMEIPENDA HII STORY
Posted on: Wed, 30 Oct 2013 06:35:44 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015