Dear Admin, Tafadhali usinitaje jina.Mimi ni binti mwenye miaka - TopicsExpress



          

Dear Admin, Tafadhali usinitaje jina.Mimi ni binti mwenye miaka 26,kwa bahati mbaya wazazi wangu walifariki nilipokuwa na miaka 8....nikashindwa kuendelea na masomo kwa kuwa hakuna mtu aliejitokeza kunisaidia kielimu. Nilipofikisha miaka 14 nilikutana na kijana mmoja aliyekuwa akiuza matunda sokoni...akajitahidi na kunirudisha tena shule,akanilipia karo zangu zote. Hivi sasa niko chuo kikuu....namshukuru mungu kwa kumtumia kuweza kutimiza ndoto zangu,tatizo ni kuwa sasa siwezi kuendelea kuwa na uhusiano nae coz si type na class yangu na pia hana elimu! Nifanyeje ili ajue kuwa sitaki uhusiano na yeye tena bila kuchoma hisia zake? Nipeni ushauri jamani...
Posted on: Sun, 07 Jul 2013 12:29:55 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015