Dola lukuki za Marekani kwenye misaada, miradi Kama nchi, Tanzania - TopicsExpress



          

Dola lukuki za Marekani kwenye misaada, miradi Kama nchi, Tanzania imesaidiwa kwa kiasi kikubwa na Marekani kupitia miradi mbalimbali Dar es Salaam. Watanzania wanasubiri kwa hamu ujio wa Rais Barrack Obama kuwa utakuwa ni neema katika harakati za kujiletea maendeleo. Ni heshima kubwa kama taifa kupokea ugeni mzito wa kiongozi wa dola lenye nguvu zaidi duniani. Kumbuka mwezi Machi Tanzania ilipokea ugeni wa Rais Xi Jinping wa China, ambayo katika siku za karibuni imekuwa na nguvu za kutisha katika medani ya uchumi duniani. China ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania, lakini katika miaka ya karibuni Marekani imetoa fedha nyingi za misaada na kuanzisha miradi mikubwa ya kuisaidia Tanzania. Marekani ni kati ya washirika wakubwa wa maendeleo kwa Tanzania kwani katika mwaka 2012 ilimwaga misaada yenye thamani ya Dola750 milioni (Sh1.2 trilioni) kusaidia shughuli za maendeleo. Nchi hiyo kupitia mfuko wa Global Fund imekuwa ikigharamia kampeni za kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria. Global Fund inafanya kazi kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Umoja wa Mataifa (UN). Pia, kuna miradi mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji, elimu, ulinzi na masuala ya ushauri katika usimamizi wa fedha. Shirika la Maendeleo la Marekani (Usaid) lilitoa Dola 350 milioni (Sh558 bilioni) kwa mwaka 2012 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, limemwaga kiasi kingine cha Dola10.5 milioni (Sh16 bilioni) kwa ajili ya ujenzi wa sehemu za kuhifadhia dawa kwa Tanzania Bara na Zanzibar. Usaid, pia imekuwa ikisaidia katika harakati za kuinua uelewa wa kinamama katika kutambua haki zao. Tayari, watu wapatao 23,000 wamenufaika kutokana na mpango huo. Katika kipindi cha miaka mitano, shirika hili limetoa kiasi cha Dola 698 (Sh1.1 trilioni) ili kusaidia katika kuimarisha sekta za usafiri, nishati na maji. Pia, Serikali ya Marekani imekuwa ikisaidia katika kuka-mbana na rushwa na hasa katika masuala ya manunuzi. Pia imekuwa ikitoa misaada mingi kwa Taasisi ya Kupambana na Kukabiliwa na Rushwa (Takukuru). Mradi wa Feed the Future (FTF) Serikali ya Marekani inaunga mkono Programu ya Tanzania ya kuinua kilimo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ili kujenga uwezo wa kujitosheleza kwa chakula. Inagharamia mpango huo kupitia mradi wa Feed the Future, ambao unafadhiliwa na ofisi ya Rais wa Marekani. Asilimia 80 ya fedha za taasisi hiyo zinagharamia mpango wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT). Mpango huo una lengo wa kupandisha kilimo katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Iringa na Rukwa. Mpango wa Partnership for Growth Rais Barrack Obama ameanzisha mpango wenye jina la `Partnership for Growth’ wenye lengo la kukabiliana na changamoto zinazokwamisha uchumi wa Tanzania kukua. Changamoto hizo kama zime za umeme na matatizo ya miundo mbinu. Mradi wa PEPFAR Mradi unaoitwa President’s Global Health Initiative (PEPFAR) unaendesha kampeni kubwa ya kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi. Tangu mwaka 2004, Tanzania imepokea Dola2.2 bilioni (Sh3.5 trilioni) kutoka taasisi hii. Pia, inaunga mkono kampeni ya kuhamasisha watu kupima ili kufahamu kama wana ugonjwa wa Ukimwi. Malaria Initiative (PMI) Mpango huu unasimamiwa na Serikali ya Marekani na ndio kwa kiasi kikubwa unasaidia kampeni ya kukabiliana ugonjwa wa Malaria nchini Tanzania. Mradi huu umesaidia kusambaza vyandaruai milioni sita kwa wanawake na watoto. Kampeni hii imesaidia kushusha maambukizi ya malaria kwa asilimia 45 kwa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano. Peace Corps Serikali ya Marekani imekuwa ikileta wafanyakazi wa kujitolea hasa katika sekta ya elimu tangu mwaka 1962. Wafanyakazi hao kupitia mpango unaoitwa Peace Corps Volunteers. Wafanyakazi hao wa kujitolea huja kwa ajili ya kusaidia katika sekta za elimu na afya. Walimu wa wanaokuja nchini huwa zaidi wa maomo ya sayansi na hisabati. Wakati wengine husaidia sekta ya afya. Ushirikiano wa sekta ya Ulinzi Wanajeshi wa Marekani hutumwa nchini kufanya kazi za kujitolea kama zile za kuchimba visima, kujenga shule na zahanati. Pia , nchi hiyo hutoa mafunzo kwa majeshi ya Tanzania ili wafanye kazi kwa ufansi kwenye kazi za kulinda amani. Tanzania hivi sasa ina majeshi katika nchi za Lebanon, Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Halikadhalika. Wamarekani hufundisha wanajeshi na polisi wa Tanzania. Kuanzia askalit 15-20 hupata mafunzo kila mwaka nchini Marekani. Benki Kuu ya Tanzania Marekani imeweka mtaalamu wake katika Wizara ya Fedha ili kushauri namna nzuri ya ulipaji madeni ya Tanzania. Mtaalamu huyo anfanya kazi na Wizara na Benki Kuu (BoT). Kubadilishana uzoefu Pia, Watanzania wapatao 20 kila mwaka huwa wananufaika na Marekani katika mpango wa kubadilishana wanafunzi na wataalamu. Mpango huu umenufaisha watu kutoka Bara na Zanzibar. Wanafunzi na wasanii wa Tanzania wamepata nafasi ya kuzuru Marekani kushiriki katika matamasha mbalimbali huko. Mifuko mingine Pia, kuna mifuko mbalimbali, ambayo inasaidia maendeleo ya Watanzania kama ule wa Mfuko wa Balozi wa Marekani wa Kulinda vivutio vya Utamaduni, pia kuna Mfuko wa Kukabiliana na tatizo la Uhamiaji Haramu na mwingine kwa ajili ya kushughulikia masuala ya demokarisa Haki za Binadamu. Mifuko yote imetoa mamilioni ya fedha, ambayo Watanzania wamenufaika nayo.
Posted on: Mon, 01 Jul 2013 09:24:41 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015