Dr. Slaa amjibu mpotoshaji mmoja wa jf kuhusu ufadhili wa - TopicsExpress



          

Dr. Slaa amjibu mpotoshaji mmoja wa jf kuhusu ufadhili wa CHADEAMA-Soma mwenyewe andiko la Dr. hapa WanaJF, Baada ya kuwaacha na kujadili kwa kina naomba sasa niwashukuru nyote mliochangia. Nawashukuru wapotoshaji kwa kuwa sasa tunawaelewa vizuri na pia tunajua dhamira zao. Nawashukuru waliojitahidi kueleza ukweli. Sasa naomba nieleze ifuatavyo: I) ni kweli Katibu Mkuu ndiye huweka mikataba mingi saini kwa niaba ya Chadema, kwa kuwa ndiye mtendaji Mkuu. 2) nadhani wote mtakumbuka kuwa mkataba na DIPD ya Denmark ulisainiwa hadharani, mbele ya Waandishi wa Habari. Sijui Hamy-D alitaka nimpelekee nyumbani kwake ili mkataba usiwe wa siri. Ni upuuzi, na kauli ya mtu asiyefikiri. Baada ya majibizano mengi nilitegemea, Hamy-D Kama Ana dhamira njema na Taifa hili angeliweka hadharani hicho anachokiita misaada ya siri. Japo angelitaja source ili watanzania wajue Kama kweli kuna misaada ya siri inapokelewa na Dr Slaa na Chadema. Bila chembe ya ushahidi ni hatari kufanyia kazi hisia tena, kwa mtu ambaye kwa muda mrefu sasa ameisha kujidhihirisha kuwa kuwadi wa ufisadi. Yote anayoandika ni uzushi, upotoshaji na uchonganishi. Watu wa namna hii ni hatari sana katika Jamii, wanapaswa kuogopwa Kama ukoma. 3) sasa ninaamini kabisa kuwa aidha Hamy-D ni mchumia tumbo, ambapo Kama ni hivyo basi ni wa kupuuzwa tu, au Ana ugonjwa sugu wa akili, unaokaribia dimentia Kama siyo kesi ya dimentia. Siku tunaweka saini mkataba na DIPD nilitaja hadharani hizo Tshs 400 million zitatumikaje. Hammy-D au Hana kumbukumbu au ni mharibifu tu kwani nilieleza kuwa fedha hizo zitatumika kujengea uwezo viongozi wetu wa ngazi mbalimbali, kuanzia Taifa, Kanda, Majimbo, Na Kata. Kwa ujumla mafunzo hayo yatanufaisha viongozi wapatao 36,000 wa ngazi mbalimbali.lengo la mafunzo hayo ni hatimaye kabla ya mwisho wa mwaka huu tuwe tumefungua matawi 18,000 yaani asilimia 100% ya. Vijiji vyote nchini na vitongoji na mitaa takriban 250,000 nchi nzima. Kazi hiyo inaendelea na sasa imefikia ngazi ya kata kwa Kanda zilizozinduliwa mapema. Kuna uwazi gani zaidi ya huo. Taarifa hiyo ilitolewa mbele ya wahisani na waandishi wa Habari, na katika nafasi mbalimbali baadaye. Misaada ya Wahisani wetu toka KAS imesaidia kuchapisha vitabu vya mafunzo hayo. Hamy-D kama angelikuwa na kumbukumbu ya mtoto wa miaka 3 angeshindwa kukumbukuka na kufuatilia kinachofanyika? Hata hivyo kwa kuwa lengo lake linaeleweka, Kama nilivyowahi kusema huyu ni wa kupuuza tu,kwani kuna watu hawaelimishiki hata ungelifanya nini. Tumpuuze Kama kawaida. Au aje na hoja yenye mashiko. source: jf
Posted on: Mon, 29 Jul 2013 09:31:59 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015