Enyi dada wakislam kwanini HAMULINDI hadhi yenu muliyo pewa na - TopicsExpress



          

Enyi dada wakislam kwanini HAMULINDI hadhi yenu muliyo pewa na ALLAH? Wallahi jambo la kusikitisha sana hili. Leo imefikia wanawake waingia dukani kununua nguo ya ndani, mwenye duka wa kiume amtolea iliyo size yake bila ya kumwambia,kama ungekuwa wajihifadhi kama dini ilivyo kuruhusu angelijuaje size ya nguo yako ya ndani? Kuna tabia mwanamke akishaona pele kuna kundi la kina Swaleh,Khamisi,basi mwendo utabadilika ghafla na kuwatolea salam kwa sauti ya kulegea. Lakini akipishana na Khadija,Fatma hawezi kumpa salam. Siku hizi kuna hizo wigi na weav basi kilaumuonaye kabandika. Tena wana waume, janaba pia aziogwi kisa zitaharibika. Ukiuliza wanadai fashion. Njoo huko saloon, kuna bandikwa nywele mtu ukimuona utadhani ngamia, kunakatwa nyusi kisha zinatiwa piko, kuna pakwa marangi ya kucha,kunabandikwa kope,lense ili awe mzungu. Wote nani hao ni madada! Kuna hizo skinjeans,pencil,pipe,skintight mtu akitaka kuvua hadi aite wenziwe wamsaidie kuvua! Wakutana na mtu miezi mitatu hamjaonana ghafla amekuwa mwarabu. Njoo uwapate njiani wamejipamba,wakajifukiza jamani eehe aifai. Mtume swala Allahu alayhi wasallam aliwaona wanawake wengi mòtoni akarudi akasema kuna watu watakuwa duniani lakini tayari wameshaingia motoni. Kina nani hao wanao mkosoa ALLAH jinsi alivyowaumba. Jamani moto wa ALLAH ni mkali aliuwasha kwa miaka 1000 ukawa mweupe akauwasha tena miaka 1000 ukawa mwekundu akauwasha tena miaka 1000 ukawa mweusi. ulimliza mtume s.a.w na maswahaba. vipi sisi tusiuogope na kulia???
Posted on: Fri, 21 Jun 2013 13:02:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015