Eti kakuku ka kawaida tu sokoni mnauza elfu kumi! Kwani - TopicsExpress



          

Eti kakuku ka kawaida tu sokoni mnauza elfu kumi! Kwani kanataga mayai yaliyochemshwa? Eti mwisho wa gari Tabata Bima, kwani likivuka Tabata Bima linabadilika kuwa meli? Eti kamkoba tu kakuninginiza mkononi (pochi la kike) laki mbili! Kwani inabeba mimba? Eti kufuli la solex shilingi elfu hamsini. Kwani linakuja na mlinzi? Eti kioo tu cha kujiangalia kwenye dressing table laki mbili na nusu! Kwani kinaona fyucha?! Eti maji ya kunywa kachupa kadogo tu buku. Kwani mmeyachota kwenye kisima cha uzima? Eti boksa buku ishirini! Kwani inakuja na saspenda za testikozi?! Eti yai shilingi mia saba. Kwani hao kuku walitagia Aga Khan hospital? Eti kioo tu cha kujiangalia kwenye dressing table laki mbili na nusu! Kwani kina sehemu ya ku-save images? Eti chipsi kavu sahani moja buku nne! Kwani mnakaanga na losheni? Eti kwenda kumuona simba mbugani ni laki tatu? Kwani amekuwa simba wa Yuda?
Posted on: Tue, 15 Oct 2013 13:17:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015