Funga inamuokoa mtu kutokana na moto *********** Kama ilvyopokewa - TopicsExpress



          

Funga inamuokoa mtu kutokana na moto *********** Kama ilvyopokewa na imam Ahmad katika Hadiyth sahihi. Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakika ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Swawm ni kinga itamukoa mja kutokana na moto (siku ya Qiyaamah) (imepokewa na At-Twabaraaniy kutoka kwa ‘Uthmaan bin Abil ‘Aas) Na katika Hadiyth iliyopokewa na ambayo ni muttafaqun ‘alayhi, inasema: Kutoka kwa Abu Sa’iyd Al Khudhriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakika Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufunga siku kwa ajili ya Allaah Mwenyeezi Mungu Atamuokoa uso wake kutokana na moto kwa umbali wa miaka sabini" Ndugu yangu Muislam ikiwa unafunga siku moja na Allaah Anakuokoa na moto wa Jahannam je, Ukifunga Ramadhaan yote! Hakika hii ni fadhila kubwa. Na fadhila hizi zinaingia katika funga za lazima na funga za Sunnah. inaendelea........
Posted on: Sat, 22 Jun 2013 14:10:30 +0000

Trending Topics



trai như Powell, không nhanh như

Recently Viewed Topics




© 2015