HABARI KUU ASUBUHI LEO Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Kwa - TopicsExpress



          

HABARI KUU ASUBUHI LEO Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Kwa Kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Watu wa Sweden SIDA Linatarajia Kuanza Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Umeme wa Makambako-Songea Unaotarajiwa Kuhudumia Zaidi ya Wananchi Laki Moja Katika Mikoa ya Njombe na Ruvuma. Katika Kuhakikisha Mradi Huo Unaanza Vema Mwezi Oct Mwaka Huu Shirika Hilo Limeanza Kutoa Elimu Kwa Wananchi wa Vijijiji Vinavyotarajiwa Kunufaika na Mradi Huo Mkoani Njombe na Kuwataka Kujiandaa Kwaajili ya Kuupokea Mradi Huo. Aidha Wananchi Hao Kupitia Mradi Huo Wataweza Kuunganishiwa Huduma ya Umeme Kwa Gharama Nafuu ya Shillingi 32,900 Katika Kipindi Hiki Cha Mradi Kabla ya Kupanda Kwa Gharama Hiyo Baada ya Kukamilika Kwa Mradi. Miongoni Mwa Vijiji Hivyo ni Pamoja na Kifanya,Lilombwi,Mikongo na Itipingi. TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
Posted on: Wed, 24 Jul 2013 03:35:49 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015