: HATA KAMA ANA WANAWAKE , NIACHENI NA PREZZO WANGU by - TopicsExpress



          

: HATA KAMA ANA WANAWAKE , NIACHENI NA PREZZO WANGU by Masha~Maphys:~Mwaija Salum MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Clouds, Loveness Malinzi ‘Diva’ ambaye hivi karibuni alianika penzi lake na mwanamuziki wa Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’, amefunguka kuwa watu waache kumsema vibaya mtu wake huyo na kudai hata kama ana wanawake wengine, anampenda tu. Loveness Malinzi ‘Diva’ katika pozi na staa wa muziki wa Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’. Diva juzikati kupitia mtandao mmoja wa kijamii alisema: “Watu wananizungumzia sana mimi na Prezzo na wengine wanasema eti ni mtu wa wanawake sana, jamani Prezzo ni rais, ni mtu mzima na labda hamumjui vizuri ila niamini mimi, jamaa ni sweetheart. Prezzo katika pozi na Huddah. “Ni mtu mzuri sana na naweza kusema nina bahati sana kuwa naye. Acheni kuzusha vitu ambavyo havipo na hata kama vipo hamna uhakika navyo. Hilo la kusema anatembea na Huddah au Victoria, namtakia kila la heri, ana baraka zangu zote na nampenda kwa kuwa ni mwanaume wa aina yake, niacheni,” alisema Diva na
Posted on: Fri, 21 Jun 2013 03:17:48 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015