HII NDIYO KAZI KUBWA YA MABALOZI WA TANZANIA WANAPOKUWA NJE YA - TopicsExpress



          

HII NDIYO KAZI KUBWA YA MABALOZI WA TANZANIA WANAPOKUWA NJE YA NCHI. Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa kazi kubwa ya mabalozi wa Tanzania katika nchi za nje ni kutetea maslahi ya nchi yao na kuijengea marafiki. Aidha, alisema kuwa ni wajibu wa kila Balozi wa Tanzania popote alipo kuonyesha sura nzuri ya Tanzania, kuvutia wawekezaji katika maeneo mbali na kutangaza nafasi nyingi za uwekezaji nchini. Alisema Tanzania ina utajiri mkubwa wa utalii duniani na ni kazi ya mabalozi hao kuutangaza hasa Marekani ambayo kwa sasa ndiyo nchi inayoongoza kwa kuleta watalii wengi nchini Tanzania. “Kazi yenu kubwa ni kulinda na kutetea maslahi na heshima ya Tanzania katika maeneo yetu ya mamlaka. Jengeni jina la Tanzania katika maeneo yetu. Itengenezee nchi yetu marafiki wa kila aina na vutieni wawekezaji kutoka kwenye maeneo yenu waje kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.” “Tunataka kuwaeleza watu wenye fedha na rasilimali za kuwekeza nchi za nje kuwa Tanzania ni nchi nzuri kupeleka mitaji yao na kuwa mitaji yao itakuwa salama.Tangazeni utajiri mkubwa wa utalii Tanzania. Tuna imani nanyi kuwa mtaifanya kazi hiyo vizuri na kwa mafanikio. Natawakieni kila la heri.” Chanzo:Ippmedia
Posted on: Sat, 21 Sep 2013 09:28:43 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015