HII NI TAARIFA MAALUMU KUTOKA OFISI YA BUNGE KUJA KWA - TopicsExpress



          

HII NI TAARIFA MAALUMU KUTOKA OFISI YA BUNGE KUJA KWA WATANZANIA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA TAARIFA KWA UMMA MKUTANO WA KUMI NA MBILI WA BUNGE Mkutano wa kumi na mbili wa Bunge utaanza siku ya Jumanne tarehe 27 Agosti, 2013 na kumalizika tarehe 13 Septemba, 2013. Mkutano huo unafuatia kumalizika kwa vikao vya wiki mbili za Kamati za Bunge kuanzia tarehe 12 Agosti, 2013. Siku ya Jumatatu tarehe 26 Agosti, 2013 kitafanyika kiako cha kupeana maelezo (briefing) na baadae kufuatiwa na Vikao vya Kamati za vyama vya siasa (Party Caucas) kuanzia saa kumi na moja jioni. Katika mkutano huu Bunge linatarajia kujadili na kupitisha miswada sita kama ifuatavyo: 1. Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa Mwaka 2013 [The National Irrigation Bill, 2013]. 2. Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2013 [The Statistics Bill, 2013]. 3. Muswada wa Sheria ya Vyama vya Ushirika wa Mwaka 2013 [The Cooperative Societies Bill, 2013]. 4. Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Akiba wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu wa Mwaka 2013 [The GEPF Retirement Benefits Bill, 2013 5. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013 [The Constitutional Review (Amendment) Bill, 2013. 6. Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa Mwaka 2013 [The Referendum Bill, 2013]. Aidha, Bunge linatarajiwa kupitisha Azimio la kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano katika Masuala ya Ulinzi (The East African Protocol on Cooperation in Defence Affairs) na Kuzindua Taarifa ya Maendeleo ya Tanzania [Tanzania Human Development Report]. Ni katika kipindi hicho kutafanyika pia Semina Kuhusu Mradi wa Vijiji vya Milenia uliopo Uyui Mkoani Tabora. Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge DAR ES SALAAM 22 Agosti 2013
Posted on: Fri, 23 Aug 2013 06:50:29 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015