HUYU NI WENGER, YULE NI HENRY, HUYU NI ADEBAYOR NA YULE PALE NI - TopicsExpress



          

HUYU NI WENGER, YULE NI HENRY, HUYU NI ADEBAYOR NA YULE PALE NI GIROUD. UTOFAUTI WAO UPO HAPA TU, YULE MVUMILIVU, HUYU ANAFUNGA ZAIDI, WALE WANAASSIST ZAIDI. Naweza kusema kwamba kwa pale Uingereza hakuna kocha ambaye ana uvumilivu zaidi ya Arsene Wenger. Huyu kocha wa kifaransa amekuwa wa kipekee sana kwa sera yake kubwa ya kujaribisha wachezaji na hata kuwapa nafasi kubwa zaidi ya kuonyesha uwezo wao. Amekuwa kocha namba moja ambaye huamini zaidi katika vijana, yeye ndiye huwafanya wale wachezaji wasio na majina wawe na majina. Hivi ulikuwa ukimfahamu Niklas Bendtner, Cesc Fabregas, Van Persie, Flamini na wengine wengi hapo kabla? Najua jibu litakuwa hapana ila walipoanza kupewa nafasi katika umri wao mdogo, wakaonyesha na kuanza kufahamika pia. Huyu ndiye kocha ambaye amebaki peke yake, kila siku anaamini kwamba vijana wanaweza kumpatia ubingwa, Wenger anaamini kwamba kuna siku Giroud atakuwa mfungaji mzuri kama Thierry Henry, Wenger anaamini kwamba kuna siku Abou Diaby atacheza kama Patrick Vieira, yes, hivyo ndivyo anavyoamini na ndio maana kila siku anawapa nafasi waonyeshe. Ukiwa kijana mdogo katika timu kama ya Arsenal, utacheza sana na ndio maana wachezaji wengi chipukizi wanataka kucheza hapo kwa ajili ya kujulikana katika ulimwengu wa soka duniani. Uvumilivu wa Wenger wakati mwingine umekuwa ukiigharimu sana timu, huo ndio ukweli. Unamkumbuka Emmanuel Adebayor? Alikuwa mchezaji ambaye aliletwa Arsenal kucheza namba kumi, labda Wenger alitaka amsaidie Henry kwani umri wake ulikuwa umesogea na hivyo asingeweza kuwa mkimbiaji kama alivyokuwa zamani. Adebayor akaletwa, akatakiwa kusaidiana na Henry kwani Dennis Bergkamp alikuwa amestaafu na hata Robin Van Persie alikuwa akikumbwa sana na majeruhi. Baada ya Henry kustaafu, mzigo wa ufungaji akapewa Adebayor. Ni nani asiyejua kwamba Adebayor alikuwa akikera? Ni nani asiyejua kwamba Adebayor alikuwa akipata nafasi za wazi mbili kati ya sita alizokuwa akiwekewa? Adebayor alikera sana na kikafikia kipindi ambacho mashabiki wakasema kwamba “IMETOSHA”. Watu wakaanza kumzomea kila alipokuwa akigusa mpira, tena hao walikuwa mashabiki wake ambao kila siku walikuwa wakimshangilia. Mashabiki kila walipokuwa wakihojiwa, walisema wazi kwamba walitaka Adebayor aondolewe. Wenger akayaziba masikio yake, kichwa chake kiliendelea kuamini kwamba Adebayor angekuwa kama Thierry Henry, hakujua kwamba Henry alikuwa akijituma sana mazoezini kwa ajili ya kufanya vizuri ila kwa Adebayor hakutaka kujituma zaidi. Angejituma zaidi ili iweje? Yupo katika klabu kubwa inayojulikana duniani, ameitwa kwenye kikosi chake cha taifa, sasa ajitume ili apate nini tena? Kuzomea kulipozidi, Wenger akaamua kumuuza. Ile ilimuuma sana Adebayor, moyo wake ukawa na kisasi, akatamani kukutana na Arsenal ili kutudhihirishia kwamba alikuwa mkali, siku alipotufunga pale Etihad, akakimbia umbali mrefu huku moyoni akisema “Leo mtakoma” alipofika katika upande wa mashabiki wa Arsenal, akajitelezesha, akauweka uso wake katika hali ya kutaka kujua kuna nani mwingine kama yeye. Huyo alikuwa Adebayor, alipewa nafasi Arsenal, akashindwa kuitumia ipasavyo. Ukiachana na huyo, kuna mwingine aliitwa Niklas Bendtner. Unamkumbuka? Alipata jina akiwa na umri mdogo pia. Alikuwa akijua kufunga kwa miguu na kichwa. Naikumbuka ile mechi na Tottenham, mechi ambayo aliingia sub kipindi ambacho tulikuwa tunapiga kona, kona ilivyopigwa, akatupia, ulikuwa mpira wake wa kwanza kuugusa. Bendtner na Adebayor hawakuwa na tofauti, yaani Adebayor alifua na Bendtner kuanika. Kama kawaida nae akakosa sana magoli ya wazi, tukaanza kulalamika kama tulivyokuwa tukimlalamikia Adebayor. Unaikumbuka ile mechi tuliyocheza na timu ya daraja la kwanza kipindi kile, Bunley katika kombe la Carling Cup? Bendtner alipewa jukumu la kuwaongoza vijana, alikosa nafasi tano za wazi kabisa. Kuanzia siku ile, kampuni ya NIKE ikampokonya viatu vya hadhi ya juu ambavyo huvaliwa na wafumania nyavu, wakampa viatu vya hadhi ya chini, unakumbuka hiyo? Wenger hakukoma, yeye alikuwa akiamini Bendtner angeweza kuwa mkali kama Henry, akaendelea kumpa nafasi kama kawaida ila hakutaka kubadilika, mwisho wa siku Wenger akagundua kwamba alikuwa akifanya kitu ambacho hakikutakiwa kufanywa, akaachana nae. MASHABIKI WANAOMSIFIA GIROUD KWA ASSIST KULIKO KUFUNGA. Kuna mashabiki sijui niwaweke kwenye kundi gani, labda kundi la watu wasiofikiria sana. Leo hii mtu anasimama mbele ya watu na kusema kwamba Giroud ni staiker mzuri sana kwa sababu anafunga na kutengeneza magoli, yaani anaassist sana kuliko kufunga. Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, tumeleta Giroud Arsenal kwa sababu anatakiwa kufunga zaidi ya kuassist, kazi ya kuassist sio yake sana, sisi tunamtaka yeye afunge kwa sana. Unamkumbuka Ronaldo De Lima, Ronaldo anajulikana kama mshambuliaji mkali ni kwa sababu alikuwa anafunga sana. Kwani Ronaldo hakuwa akiassist? Leo hii ni nani anakumbuka kwamba Ronaldo alikuwa akiassist sana? Hakuna, tunachokikumbuka ni kwamba Ronaldo alikuwa akifunga sana. Mfuatilie na Henry, unaikumbuka ile mechi ya Arsenal na Southampton iliyochezwa tarehe 17 May 2003? Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kabisa kati ya zile 49 ambazo hatukufungwa. Mechi ile, Thierry Henry aliassist magoli matatu, nani anakumbuka hilo? Nadhani hamkumbuki kabisa. Nimekukumbushia mechi hiyo ni kwa sababu nataka ujue kwamba assist huwa hazikumbukwi kwa forward, mchango mkubwa wa foward unakumbukwa pale anapofunga tu. Assist hazikumuweka Henry juu yapokuwa mwaka 2003-2004 ndiye alikuwa mchezaji aliyeongoza kwa assist nchini Uingereza. Leo hii tunamkumbuka Henry kwa magoli yake na hivi ndivyo inavyotakiwa kufanywa na Giroud. Kaitwa kwa ajili ya kufunga sana na si kuaassist. Mtoto wako atakapokuuliza baadae kwamba “Baba hivi Giroud alivyoichezea Arsenal alikuwa akifunga sana?” Hapo kumbuka kwamba jibu utakalolitoa halihusiani na assist, mtu anajua kwamba Giroud alikuwa mfungaji hivyo alitakiwa kuzungumziwa kuhusu ufungaji wake kwani mambo ya assist hutokuwa nikiyakumbuka, hivyo ndivyo vinavyotufanya assist za Henry, Ronaldo tusikumbuke zaidi ya ukali wao wa kufumania nyavu. Giroud bado kabisa, narudia tena kwamba uwezo wake ni wa mchezaji wa kuchezea timu ndogo, timu kubwa ina presha sana na watu wanataka kila wakati uwe unafunga kila unapopata nafasi. Mshambuliaji hasifiwi kwa assist kwani hizo husahaulika katika ulimwengu wa soka, mshambuliaji hukumbukwa kwa kufumania nyavu tu. Leo hii Ozil anapoassist goli tatu tunamuona mkali, kwa nini sasa mafoward wengine wanaoassist goli nne tusiwaone wakali? Hapo ni lazima ukumbuke kwamba kuassist ni moja ya jukumu alilopewa Ozil na ni lazima alifanyie kazi, kwa Giroud tunataka afunge tu, hata akiwa mchoyo, acha awe mchyo lakini tunataka afunge. Mtazame mshambuliaji kama Suarez, ni mchezaji mchoyo sana afikapo ndani ya kumi na nane ila pamoja na uchoyo wake, anafunga. Hivi utaweza kusimama na kusema Suarez mchoyo? Hauwezi kwa sababu jukumu alilopewa analifanyia kazi. Mtu kama Thierry alitutosha, alipokuwepo hatukuwa tukililia foward mwingine aje japokuwa Wenger alikuwa akituletea tu ila sisi hatukuwa na uhitaji nao kwani Henry alionekana kutosha sana. Leo hii, mashabiki wa Arsenal tunataka aletwe foward wa kumhamasisha Giroud, kwa nini kipindi kile hatukutaka aletwe foward wa kumhamasisha Henry? Henry alijitosheleza sana na alikuwa akifanya kazi kama alivyotakiwa kuifanya. Ukali wa Henry ndio unaotufanya Giroud kumuona galasa, kama Henry asingekuwa amecheza Arsenal basi leo tusingekuwa tukilalamika kuhusu Giroud, ila kwa sababu mtu mkali amepita pale basi na sisi tunataka Giroud awe mkali. Wakati Arsenal inacheza na Tottenham tarehe 22/04/2006, Arsenal alihitaji suluhu ili aweze kufuzu kwenda ligi ya mabingwa ulaya na hiyo ndio ilikuwa mechi moja ngumu kati ya tatu zilizokuwa zimebakia. Sijui Wenger aliona nini, katika mechi ile, Henry alikuwa bench, Adebayor kama kawaida yake alikuwa akirukaruka tu pale mbele. Wakati wa kipindi cha pili Henry alipokuwa akiingizwa, kamera zikawachukua mabeki wa Tottenham, walionekana kuchoka sana, yaani uingiaji wa Henry ukaonekana kuwachosha sana na kujua kwamba moto usiozuilika ulikuwa ukiingia. Na kweli, dakika kadhaa toka aingie, Henry akafunga goli zuri la kusawazisha zikiwa zimebakia dakika kumi mpira uishe huku assist ikiwa imetokea kwa Emmanuel Adebayor. Goli lile la Henry tunalikumbuka lakini unaikumbuka assist ya Adebayor? Bila shaka hauikumbuki. Giroud amekuwa tofauti sana na foward tunayemtaka pale Arsenal, hana control, nadhani hapo haubishi, hana uhakika na anachokifanya na pia hupoteza mipira sana kitu kinachokasirisha kupita kawaida. Hakuna beki anayemuogopa Giroud kwa sababu uwezo wake ni wa chini sana. Msimu uliopita, yeye kama foward alifunga sijui goli 22 msimu mzima. Hebu mwangalie Thierry Henry, alipokuja Arsenal kutoka Juventus Wenger alimwambia acheze foward, yeye akasema hivi, namnukuu “Nimecheza Monaco nikiwa kama winga, nimecheza Ufaransa pia nikiwa winger na hata Juventus kwa mechi chache nilizocheza nilikuwa winger na duniani ilinitambua kama winger. Kitendo cha kocha kuniambia kwamba aliacha kumsajili Ronaldo de Lima kwa ajili yangu alinishangaza sana, alijua fika kwamba Anelka aliondoka, akaniambia kwamba mimi natakiwa kuwa foward. Hilo lilikuwa jambo gumu sana, nilimwambia kwamba siwezi kufunga, yeye akaniambia wewe cheza kama forward na utajua kufunga, na kweli nikajaribu japokuwa mechi mbili za kwanza nilikosa sana magoli kwa kuwa sikuzoea” Pamoja na maneno hayo, pamoja na kujifundisha kuwa foward, Henry alifunga magoli 26 msimu mzima, msimu wake wa kwanza. Kwa kifupi, Henry alikuwa na kipaji cha kufunga. Kwa Giroud mambo yamekuwa tofauti sana, yeye kasajiliwa kama foward, huko alipotoka alikuwa akicheza kama foward lakini magoli yake ya msimu mzima wa kwanza hakuweza kuyafikisha magoli ya Henry, hapo jua kwamba Giroud kama Giroud hana kipaji cha kufunga. Zitazame timu nyingine, kuna Suarez, kuna Aguero, Van Persie, kuna Ibrahimovich na wengine wengi, wakisimamishwa hao hivi utamuweka Giroud na kusema kwamba yeye nae yupo juu? Naikumbuka mechi ya Beyern msimu uliopita. Nyumbani kwake tulimkamata vizuri, tukamfunga mbili, dakika ya 89 Giroud anapokea mpira mzuri wa kumwambia Bayern itakubidi ubaki na usiendelee, mchezaji yule, jamaa yule anayependa kutoa ulimi kama kenge, anakosa goli la wazi na kubaki akishika kichwa tu, alinikera sana. Kwa sasa hivi mashabiki tushajua kwamba yeye si mkali na ndio maana tunataka foward wa ukweli. Naomba uniamini nikwambiacho kwamba akija kutua foward mkali, huo ndio utakuwa mwisho wa Giroud. Hii ni kwa sababu tutakuwa tunakipata tunachokitaka, Giroud atakuwa na umuhimu gani tena? Wenger anamvumilia, sawa ila kuna siku sisi mashabiki tutamchoka, tutamzomea kama tulivyofanya kwa Adebayor na mwisho wa siku tutashinikiza auzwe kwani haufanyi wajibu wake uwanjani, kazi yake kuingilia wajibu wa kina Ozil na wajibu wake anamuachia Ramsey. Kama unakumbuka vizuri basi nadhani utaikumbuka mechi ya Arsenal na Manchester United ya mwaka 1999 bila shaka, tena ilikuwa fainali ya F.A. Hakuna siku ambayo tulicheza mpira wa pasi na kasi kwa Manchester kama siku hiyo. Tulimchezea sana, aliutafuta mpira kwa tochi. Dakika ya 90 tukapata penati, Bergkamp akapiga, akakosa, mpira ukaisha na dakika kuongezwa. Naikumbuka mechi ile, Giggs akapangua mabeki kadhaa na kukutana na David Seaman, wakati Seaman anapiga magoti chini, Giggs akapiga kwa juu. Giggs akavua fulana yake, akaanza kuipepea juu, manywele yake kifuani yalikuwa makubwa, hakuonekana kujali, Manchester akatufunga, akachukua kombe. Sasa hivi unadhani mtu akija kuniuliza kuhusu mshindi wa mechi hiyo nitasema kwamba tulimfanya Man U autafute mpira kwa tochi? Nitaonekana kuwa sina akili, watu wanaangalia matokeo. Na hivyo ndivyo inavyotokea kwa forward, watu baadae hawaangalii assist, watauliza tu, je alikuwa akifunga sana? Assist hukumbukwa wiki moja baada ya mechi, baada ya hapo husahaulika. Kwa wale wanaozifurahia assist za Giroud, natumaini miaka ya baadae watakapoulizwa kuhusu Giroud alifanya nini watawaambia watoto wao kwamba alikuwa akitoa assist nyingi sana...hahahaha! Huo ni ujinga na inaonyesha kwamba haujielewi na hata mtoto wako ataona kuwa baba kapagawa kwa sabbu uzee unamuendesha puta. Foward unatakiwa ufunge, mambo ya kukaa mechi tatu bila kufunga sisi hatutaki, usituletee mambo ya kuassist hapa, sisi tunataka ufunge ili tumsahau Henry wetu. Kama ingekuwa kuassist ni dili sana kwa foward, basi hata sanamu la Henry lingetengezwa akionekana akiassist, lakini ukiliangalia, limetengenezwa akiwa anashangilia, hapo ndio ujue huo ulikuwa ni wajibu wake kila anapokuwa uwanjani. Nadhani anayemsifia sana Giroud kwa kuassist kuliko kufuga, huyo ndiye shabiki mamluki ambaye hakuwahi kuishangilia Arsenal wakati henry yupo, kwa hiyo kwake assist ni bora zaidi ya kufung kwa foward. Acha sisi tuliyoyaona makli ya Henry tuendelee kupiga kelele mapungufu makubwa aliyonayo Giroud. NB: NAFIKIRI KAMA SUAREZ, VAN PERSIE, ROONEY, AGUERO, TORRES, IBRAHIMOVICH, FALCAO WANGEZUNGUKWA NA WACHEZAJI WA KUASSIST KWA IDADI KUBWA KAMA YA ARSENAL YAANI OZIL, RAMSEY, JACK, CAZORLA NA ROSSICKY....LEO HII WANGEKUWA NA MAGOLI ZAIDI YA 20 KWENYE LIGI ILA KWA GIROUD NDIO KWANZA ANA MAGOLI 5 NA ASSIST ZA KUMWAGA. WENGER HEBU TULETEE SUAREZ ILI GIROUD AUKUMBUKE WAJIBU WAKE UWANJANI. COYG
Posted on: Sun, 27 Oct 2013 19:51:50 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015