Habari za asubuhi, umeamka je hapo ulipo? sisi hapa hatujambo, uko - TopicsExpress



          

Habari za asubuhi, umeamka je hapo ulipo? sisi hapa hatujambo, uko nami Ali Bilal kukujuza yanayojiri asubuhi hii, ambapo tunahabari kuhusu: Serikali ya Uganda imekiri kumshikilia kiongozi wa kijeshi wa kundi la M23 Sultani Makenga na kusisitiza kwamba haina mpango wa kumsalimisha mpiganaji yeyote kwa serikali ya Kinshasa. Nchi ya Tanzania imeendelea kusisitiza kuwa yenyewe sio chanzo cha kukwamisha maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba hata kama baadhi ya viongozi wa nchi wanachama wanaitenga haitabadili msimamo wake kuhusu mambo ya msingi ya Jumuiya hiyo. Serikali ya Ufaransa inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika wa mauji ya waandishi wa habari wawili raia wa Ufaransa, licha ya kundi la Aqmi nchini Mali kukiri kuhusika na mauaji hayo. Wakuu wa mashirika ya ujasusi nchini Uingereza M15, M16 na GCHQ wameonya kuhusu makundi ya kigaidi duniani kutumia taarifa za siri zilizovujishwa na jasusi wa zamani wa Marekani Edward Snowden katika kupanga na kutekeleza vitendo vya kigaidi. Tutumie maoni na utwambiye upo wapi
Posted on: Fri, 08 Nov 2013 04:26:18 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015