Hapana chezea mimi....nimezaliwa enzi hizo kumbi za harusi - TopicsExpress



          

Hapana chezea mimi....nimezaliwa enzi hizo kumbi za harusi zinapambwa kwa toilet paper na kanga.... Enzi hizo safari ya Dar-Mbeya ni siku mbili.... Enzi hizo kina dada wanachoma nywele kwa chanuo la chuma... Enzi hizo ushindani wa soka ulihusisha Reli Morogoro, Milambo Tabora, Ushirika Moshi....yaani walikuwa wababe wa Simba na Yanga.... Enzi hizo mtu akiwa na radio ya double cassette ilikuwa stori mtaa mzima... Enzi hizo mwenye Peugeot 504 ndo alikuwa tajiri ile mbaya.... Enzi hizo stendi kuu ya mabasi ya mikoani ilikuwa pale Kisutu.... Enzi hizo hakuna mkoa wa Dar es Salaam....Dar yenyewe ilikuwa ndani ya mkoa wa Pwani. Enzi hizo ukipiga picha unasubiri mwezi mzima mkanda ujae ndo picha zikasafishwe studio.... Enzi hizo mwanasiasa aliyekuwa anapendwa na kusikilizwa kuliko wote alikuwa anaitwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.... Enzi hizo Jakaya Kikwete ni katibu wa CCM wa wilaya.... Enzi hizo shushushu aliyeogopwa zaidi alikuwa ni balozi wa nyumba kumikumi... Enzi hizo kuagiza barua kwenye mabasi ndo ilikuwa mtindo wa mawasiliano... Halafu wewe umezaliwa hayo mambo yote hayapo na bado unataka kuniletea za kuleta. Wa wapi wewe?
Posted on: Mon, 02 Sep 2013 09:40:24 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015